Mifugo ikiwa imekufa kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Kahama mkoani Shinyanga.
Mabaki ya nyumba zilizochukuliwa na mafuriko Wilayani Kahama.
Mabaki ya nyumba zilizosombwa na mafuriko.
Na Mweandishi Wetu
MAFURIKO Makubwa yametokea usiku wa kuamkia leo mkoani Shiyanga na kuua watu 38 na nyumba zaidi ya 110 zikiwa zimechukuliwa na maji na kusababisha maelfu ya wakazi kukosa makazi ya kuishi.
Mbali ya mvua hiyo kuua watu 38, mvua hiyo imeua mifugo kadhaa ambapo Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige ameziomba taasisi mbalimbali za kiserikali
na zisizo za serikali kujitokeza na kutoa msaada wa hali na mali kutokana na maafa yaliyotokea jimboni kwake
ili wakazi hao waweze kujikimu na kujipanga
upya na maisha.
“Nimezungumza
na mkurugenzi ameniambia mvua kubwa imenyesha kuanzia majira ya saa nne
usiku hadi majira ya saa 11 zikiambatana na upepo mkali na barafu
zilizosababisha madhara hayo,” alisema.
Alisema waathirika hao kwa sasa wanahitaji zaidi msaada kwa majeruhi, ambao ni wa makazi na chakula, huku akielezea kuwa mali zilizoharibiwa ni pamoja na makazi pia mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku.
No comments:
Post a Comment