KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC Joseph Omog na
Msaidizi wake Ibrahim Shikanda, wametimuliwa rasm kuinoa timu hiyo kutokana na
kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba wao.
Habari ambazo Habari Mseto imezipata hivi punde,
kocha huyo na msaidizi wake wametimuliwa kutokana na kukiuka kipengele cha
kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya michuano ya Kimataifa ambapo
Azam FC ambao ni Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara waliondolewa na El
Merreikh kwa kubugizwa mabao 3-2 baada ya nyumbani kushinda 2-0 huku ugenini
wakichapwa bila huruma 3-0.
Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Saad
Kawemba alithibitisha kutimuliwa kwa makocha hao, na kusema kuwa, wamekiuka
masuala ya kimkataba.
“Tumevunja mikataba yao, na mazungumzo
tumeyafanya, na kukubaliana, hivyo basi hakuna wa kumlaum mwenzake kwani wao
wamekiuka mkataba,”alisema na kuongeza kuwa George Nsimbe ndiye atainoa timu
hiyo mpaka ligi kumalizika.
Kutokana na timua timua hiyo nafasi ya Mcameroon
huyo inatarajiwa kuzibwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Patric Liewig.
No comments:
Post a Comment