HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2015

Tamasha la Pasaka 2015 kuwabeba Free Media

Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Khamis Pembe akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama.

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Msama Protions inayoendesha Tamasha la Pasaka imekubali kufadhili maandalizi ya timu ya soka ya Free Media pamoja na ile ya netiboli zinazotarajiwa kushiriki mashindano ya Kombe la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF MEDIA CUP).

Akizungumza na Meneja wa timu hiyo, Saleh Mohamed, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema lengo la ufadhili huo ni kuziwezesha timu za Freemedia kufanya vizuri katika mechi zake.
  
Msama alisema anaamini ufadhili huo utakuwa chachu ya ushindi wa timu za Freemedia dhidi ya wapinzani wao. Alisema ufadhili wake utagusa vifaa, gharama za usafiri na matumizi madogomadogo kulingana na mahitaji ya timu husika.

Msama alisema Tamasha la Pasaka limekuwa likikusanya watu wa rika na dini tofauti kumshukuru mungu na mapato yanayopatikana hupelekwa kusaidia yatima, wajane na wenye mahitaji mbalimbali.
 "Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kile anachotuwezesha".  
Msama kifafanua jambo.

Tamasha la Pasaka ni sehemu ya kuwaunganisha Watanzania na kusahau tofauti zao za kidini, kisiasa na kikabila....tunapenda wananchi wadumishe amani, umoja na mshikamano vilivyopo" alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages