HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2015

Alikiba, Diamond Platinumz vitani KTMA 2015

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza wateule wanaowania tuzo za muziki za Kilimanjaro (KTMA 2015). Kulia ni Mratibu wa Matukio kutoka Baraza la Sanaa Tanzania Basata, Kurwijira Maregesi na Mratibu wa Kitengo cha Taarifa cha kuchagua washindi, Pavel Gabriel. (Picha na Francis Dande)


Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium Lager, jana wamewatangaza wateule ‘nominees’ wa vipengele ‘categories’ 32 vya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (KTMA 2014, ambao watapigiwa kura kuanzia Mei 4 na kufikia tamati Juni 5 mwaka huu.


Hafla ya kuwatangaza wateule hao ilifanyika jana jijini Dar es Salaam, ambako mchuano mkali unatarajiwa kuwapo katika kategori tano zinazowahusisha mahasimu wa muziki wa kizazi kipya nchini ‘Bongo Fleva,’ Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ na Ali Kiba ‘Alikiba.’

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli, alisema kuwa akademi ilipitia mapendekezo ya wasanii hao ilikaa wiki iliyopita na kufanya kazi ngumu na nzito kuteua wasanii, watayarishaji kazi za wasanii na watunzi hao.

Katika KTMA 2015, Alikiba amempiku Diamond Platinumz kwa kuwania tuzo sita, dhidi ya tano zinazowaniwa na hasimu wake huyo maarufu pia kwa jina la Dangote.

Tuzo wanazowania kwa pamoja Alikiba na Diamond ni; Mtumbuizaji Bora wa Muziki wa Mwaka – Kiume, Mwimbaji Bora wa Kiume – Bongo Fleva, Mtunzi Bora wa Mwaka – Bongo Fleva, Video Bora ya Muziki ya Mwaka na Wimbo Bora wa Afro Pop.

Ukiondoa tuzo hizo, Alikiba anawania pia tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka, ambako Mwana Dar es Salaam ya nyota huyo inachuana vikali na Nani Kama Mama ya Christian Bella, Gere ya Weusi, Nitasubiri ya Juma Jux ‘Jux’, Bongo Hip Hop ya Farid Kubanda ‘Fid Q.’

Katika kinyang’anyoro hicho, Nani Kama Mama imembeba Bella kuwania tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka, Wimbo Bora wa Zouk/Rhuma, huku mkali wa ‘rusha roho’ Mzee Yusuf na nyota wa Bongo Fleva, Jux wakiwania tuzo nne tofauti. Vanessa Mdee naa Lady Jaydee kwa upande wao wakiwania tuzo nne nne.

Wadau na mashabiki wa muziki nchini wametakiwa kutumia kipindi cha mwezi mmoja kilichotangaza, kuwapigia kula wateule hao, kupitia njia nne za WhatsApp katika namba 0686 528 813, ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenda namba 15415 au mtandao wa www.ktma.co.tz.

No comments:

Post a Comment

Pages