Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akikabidhi mashuka kumi kwa Khatib Said mwenyekiti wa kijiji cha Chumo Wilayani Kilwa mkoani Lindi yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya zahanati ya kijiji hicho wakati wa mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF inayotolewa na NHIF, Ambapo wananchi mbalimbali walipima afya kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kujiunga na huduma hiyo kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Chumo, Katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi B. Fortunata Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHUMO-KILWA) Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akipongezwa na Khatib Said Mwenyekiti wa kijiji cha Chumo Wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya kukabidhi mashuka kumi yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya zahanati ya kijiji hicho wakati wa mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF Hatbal Badru mtaalam maabara akiendelea kuwapima afya wananchi mbalimbali wakati wa utoajiwa huduma hiyo. Kikundi cha waigizaji kikitoa maigizo kama mafunzo kwa wananchi juu ya umuhimu wa huduma za CHF. Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo Salvatory Okum Afisa Matekelezo kutoka makao makuu ya NHIF akizizitiza jambo wakati akihamasisha wananchi kujiunga na huduma za Afya ya Jamii CHF Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo Abdul Gaucho wa kijiji cha Chumo Uso kwa Uso na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog. Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akijadiliana jambo na Mwanaisha Lindu Diwani wa Viti maalum Kilwa wakati alipotembelea na kujionea shughuli za uhamasishaji wananchi wa kijiji cha Chumo kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akishiriki kuchezo ngoma ya Wamatumbi wilayani Kilwa. Wananchi wakiwa wamejipanga kwenye mstari tayari kwa kupima afya zao. Paul Marenga Afisa Matekelezo mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi akimpima urefu Bi. Mwanaisha Lindu Diwani wa viti maalum wilaya ya Kilwa wakati wa kampeni hiyo. Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akizungumza na wananchi wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo. Mwalimu Chatherine Ngeleja wa shule ya Msingi Chumo kulia na ndugu yake Beata Ngeleja wakisubiri kupata huduma wakati wa kampeni hiyo. Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akihamasisha wananchi kujiunga na huduma ya afya ya jamii CHF wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo.
April 28, 2015
Home
Unlabelled
NHIF YAENDELEA NA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA CHF KATIKA KIJIJI CHA CHUMO KILWA
NHIF YAENDELEA NA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA CHF KATIKA KIJIJI CHA CHUMO KILWA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment