Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Kata ya Masaki Wilayani Kisarawe Bwana Mohamed Shomoi Mlembe akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu kuzundua Rasmi Shindano la mama shujaa wa chakula 2015 msimu mpya , pamoja na wageni wote waliofika katika sherehe Hizo.
Mgeni Rasmi katika Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizundua Rasmi Shindano hilo, na kuwasihi wakinamama wa Kisarawe wachukue fomu za kushiriki kwa wingi, pia aliwashukuru Shirika la Oxfam kwa kukichagua kijiji cha Kisanga kuwa wenyeji wa Mashindano hayo.
Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea Historia na Madhumuni ya shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Diwani wa wa kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akishukuru shindano la Mama Shujaa wa Chakula kufanyika katika kijiji cha kisanga na kuwahakikishia washiriki wote kuwa kijiji kipo salama na watashirikiana pamoja kwa mambo yote wakati wa shindano hilo.
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dk. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
Baadhi ya wanakijiji cha Kisanga wakiwa katika Sherehe hizo za Uzinduzi wa Mama Shujaa wa Chakula.
No comments:
Post a Comment