Ujumbe wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC ukiwa eneo
linalomilikiwa na NHC ambalo ujenzi wa
Mji wa kisasa umeanza wakionyeshwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James
Kisarika chemchemu za maji yanayotiririka walipotembelea eneo hilo lenye hali
ya hewa ya aina yake Jijini Arusha jana.
Usariver ni Arusha Tanzania ambapo NHC Shirika lenye dhamana ya kujenga
nyumba bora hapa nchini limeanza kupanga mji huo wenye mandhari na hali ya hewa
ya kuvutia. Hapa wajumbe wa Bodi ya NHC na watendaji wa NHC wanafurahia mpango
wa kuendeleza eneo hilo lenye ekari 300 linalomilikiwa na NHC.
Hii ndiyo hatua ya ujenzi iliyokwishafikiwa hivi sasa katika ujenzi wa
nyumba za gharama ya kati aina ya “town houses” zinazojengwa na NHC Wilayani
Monduli kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment