HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2015

C-SEMA:BAJETI YA WATOTO IONGEZWE KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

 Mratibu wa utetezi na ushawishi wa SOS nchini, John Batista akitoa maada katika  Semina iloyowashirikisha wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari za watoto(TAJOC),Watunga sera na watoa maamuzi kutoka Wizara mbalimbali katika kujadili masuala ya watoto iliyofanyika katika hoteli ya Regence jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waandishi wa TAJOC,Watunga sera na watoa maamuzi kutoka Wizara mbalimbali  wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Hotel ya Regence jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya waandishi wa TAJOC,Watunga sera na watoa maamuzi kutoka Wizara mbalimbali  wakiwa nje ya Hoteli ya Regence jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SHIRIKA lisilo la kiserikali la C-Sema limeiomba serikali kuongeza bajeti  ya watoto ambayo iko wazi pasipo kuunganishwa na bajeti  nyingine   ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.
Mratibu wa programu na Uhamasishaji wa Shirika hilo, Michael Kehongoh aliseyasema hayo jijini Dar es Salaam katika semina iloyowashirikisha wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari za watoto(TAJOC) na watunga sera na watoa maamuzi kutoka wizara mbalimbali katika kujadili masuala ya watoto.

Amesema  lengo lao ni kuona mabadiliko yanaletwa ndani ya Jamii kupitia watoto na kuona wazazi na walezi wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha haki za watoto zinatekelezwa na kuleta matokeo chanya.
“Watoto wakipewa nafasi ya kusema na kushirikishwa wanaweza kuleta mabadiliko chanya  ni sasa C-Sema tunafanya programu tatu ambazo zinawashiriki watoto ikiwemo ya sanduku la maoni shuleni"alisema.
Amesema kwa sasa kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la SOS wamezindua kampeni ya 'NIJALI'  kwa ajili ya kukutana na wadau wa masuala ya watoto ili kuishawishi serikali kuongeza bajeti katika masuala ya watoto na kuhakikisha fedha zilizotengwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mratibu wa utetezi na ushawishi wa SOS nchini, John Batista kampeni hiyo inafanyika katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,  Iringa, Zanzibar na Mwanza.
Amesema Shirika hilo linajishughulisha na masuala mbalimbali ya watoto hasa katika kuweza kwenye elimu sambamba na kuimarisha makazi ya watoto.

No comments:

Post a Comment

Pages