HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2015

Chadema Kukomba Wabunge 5, Madiwani 16 wa CCM?

Na Bryceson Mathias, Morogoro

JINSI Upepo wa kisiasa unavyokiendea Kombo Chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Morogoro, kimejigamba kitakomba Wabune Watano (5), na Madiwani 16, watakaotimkia Chadema wakidai kuchoshwa na Rushwa inayofanywa katika mchakato wa kuwania nyadhifa hizo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Katibu wa Chadema Morogoro, Samwel Kitwika, alisema, Rushwa, Ukiritimba na Mchezo Mchafu uanaoendelea ndani ya CCM Morogoro kuwapata wawakilishi hao, ndiyo Mtaji na Mvuto, utaowakimbiza CCM na kutaka kutimkia Chadema.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuwataja Wawakilishi hao, Kitwika alisema,”Kwa sasa hatuwezi kuwataja Wabunge na Madiwani hao, maana ni sawa na kumuonesha adui mbinu zako, isipokuwa ifahamike wanatoka katika Majimbo yote 10 ya Mkoa wa Morogoro na Kata zake.

 “Sababu kubwa inayotangulia katika kufikia maamuzi hayo, ni Umaarufu wa Chadema tangu ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya hadi Msingi, vikiunganisha na Uadilifu na umoja ndani ya Chama, vinavyopelekea, kudhibiti Rushwa, Ufisadi na Maovu mbalimbali nje na ndani ya Chama”.alisema Kitwika.

Kitwika aliongeza kwamba, awali walikuwa na madiwani 10 waliofika kwenye ofisi za Chadema kuomba kuungana na Chama kulileta Taifa ukombozi wa kweli kwa wananchi walioumizwa na Rushwa na Maovu, lakini wiki hii, wameongezeka Madiwani Sita, na kufanya wafikie 16.

Mmoja wa Madiwani wa Moja ya Kata za Jimbo la Mvomero (Jina linahifadhiwa) alisema, “Kutokana na Malumbano ya yeye na Chama chake katika eneo la kufanywa Mhuri (Rubber Stamp) wa kupitisha Maovu, wanipitishe/Wasinipitishe, naondoka na watu wangu kwenda Chadema”.alisema Diwani huyo.

Awali Chadema kilimwaga Watia Nia wanaowania Ubunge na Udiwani katika Majimbo na Kata zinazoshikiliwa na CCM, ambapo waliwasha Moto wa kutoa Elimu na kuwajengea Uwezo watu, juu ya Nia ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA, kutwa Dola, na kuwaatia Neema.

Aidha mmoja wa Viongozi Wakongwe wa CCM Mkoa wa Morogoro aliyeomba asitajwe jina gazetini alisema, Kauli ya Chadema ni sawa na mtu anayeota na kulala usingizi akiwa juu ya Mti, ambapo akidondoka, hupoteza Maisha yake.

No comments:

Post a Comment

Pages