Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta akicheza sambamba na Mkurugenzi wa kituo cha Radio 5 Robart Francis staili ya shikorobo juzi kwenye party ya usiku wa marafiki wa Lowassa ulifanyika katika ukumbi wa triple A jijini Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Kundi la marafiki wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement”wakishangilia katika party hiyo
Katibu mwenezi wa CCM mkoani Arusha, Isack Joseph maarufu kama "kadogoo"akicheza na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta katika party ya usiku wa marafiki wa Lowassa uliofanyika katika ukumbi wa Triple A jijijni Arusha nakuhudhuriwa na watu mbalimbali
Kada maarafu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akishow love na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta katika usiku wa marafiki wa Lowassa iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha
Mwanabloga wa libeneke la kaskazini Woinde Shiza akishow love na Deo Gee mfanyakazi wa kituo cha Radio 5 jijini Arusha
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta na mwenzake,Abdulwaheed Sykes”Dully Sykes”juzi wametangaza rasmi kumuunga mkono mgombea anayetajwa kuwania nafasi ya urais kupitia CCM mwaka huu,Edward Lowasa.
Wasanii hao walitangaza uamuzi wao katika ukumbi wa burudani wa triple A uliopo jijini Arusha wakati walipokuwa wakiburudisha onyesho la marafiki wa Lowasa maarufu kama”Friends of Lowasa white Party”.
Akitangaza uamuzi wake,Sykes alisema kuwa yeye amemua kumuunga mkono Lowasa katika mbio za urais kwa kuwa ndiye chaguo lake tangu hapo zamani.
“Jamani mimi namuunga mkono Lowasa yeye ndiye chaguo langu tangu zamani mimi ni mfuasi wa kiongozi huyu”alisema msanii huyo na kuibua shangwe
Hatahivyo,kwa upande wake Billal alisema kuwa yeye atamuunga mkono mgombea huyo anayetajwa kuwania nafasi ya juu katika medani za siasa hapa nchini endapo akipitishwa na chama chake.
Alisema kuwa kila binadamu ana mapenzi yake na kwa maana hiyo yeye atamuunga mkono Lowasa kwa kuwa ndiye changuo lake kwa sasa.
Katika onyesho hilo lililoanza majira ya saa 10.00 usiku watu mbalimbali kabla ya kuwasili ukumbini walipata fursa ya kupiga picha katika zulia jekundu ambapo usiku huo ulipambwa na vazi jeupe ambapo watu mbalimbali walivalia vazi hilo.
No comments:
Post a Comment