CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM), kinadaiwa kuvunja Sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za
mitaa, kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwashawishi wananchi wa
Kijiji cha Mtambani Kata ya Bwiringu, Chalinze mkoani Pwani, kukichagua chama
hicho.
Kijiji hicho
kinatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa kesho, baada ya ule
uliyofanyika Desemba 14 na 21 mwaka jana kukumbwa na dosari lukuki
zulizosababisha kuahishwa kwa uchaguzi huo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutokea katika jimbo hilo la Chalinze, Katibu wa Operesheni, Mikakati, Propagandi na Mafunzo Mkoa wa Pwani wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Mwipopo, alisema wanafuatilia kwa
karibu ukiukwaji huo wa sharia.
Aliitaja sheria
hiyo kuwa ni ile ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na
vitongoji sura namba 287 kifungu cha 201(A), tangazo la serikali namba 320 la
5/9/2014 pamoja kifungu cha 18.
Mwipopo, alisema
kifungu hicho cha 18 kinaeleze kinakataza ngombea au chama kujihusisha kampeni
zinazoashilia vitendo vya rushwa, kashfa, ubaguzi wa kijinsia, udini na ukabila.
Alisema pamoja na
sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa wazi, Mei 11 mwaka huu
CCM kilizindua kampeni zake, ambapo walitoa fulana, jezi na mipira katika shule
na wananchi ikiwa ni kuwashawishi ili waweze kukichagua chama hicho kwenye
uchaguzi huo.
“Pia waliendelea
kuvunja kanuni hizo kwa kuwaambia wananchi wa kijiji cha mtambani kwamba
wakikichagua Chadema watawafukuza wafugaji wote, niwaombe wafugaji kuzipuuza
kauli hizo kwani Chadema ni chama makini ambacho kazi yake kubwa ni kupigania
haki za wananchi wote bila ya kubagua popote pale nchini,”alisema Mwipopo.
Alisema Chadema
siyo chama cha kibaguzi wala kikabila bali ni chama cha wananchi kutoka maeneo
yote ya Jamhuri ya Muungano, hivyo wanaokifananisha na udini na ukabila ni watu
waliofilisika kisiasa.
Katibu huyo,
alisema kuwa wananchi wa Mtambani hawahitaji fulana, mpira bali wanahitaji
barabara, maji na huduma bora za afya, ambazo CCM, imeshindwa kuwafikishia
tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1964.
No comments:
Post a Comment