Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mdororo wa shilingi. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.
Na Mwandishi Wetu
WADAU
wa maendeleo nchini hususan wanasiasa, wametakiwa kuacha tabia ya kuishinikiza
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kudhibiti mdororo wa shilingi ya Tanzania, kwani
si njia sahihi na badala yake waache thamani ya fedha hiyo kukua kulingana na mahitaji
ya kiuchumi.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei,
alipozungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania na kusema
mashinikizo kutoka kwa wadau hao yanaziathiri taasisi za kifedha, hususan
benki.
Dk.
Kimei alisema shinikizo hilo linailazimu BoT kuziminya benki, kwani njia nzuri
inayotumiwa na taasisi hiyo katika kuzuia anguko hilo na mabadiliko ya fedha za
kigeni ni kubana sera za kifedha na kuondoa zaidi shilingi katika mzunguko
wake.
“Moja
ya athari za kuondoa shilingi katika mzunguko wake ni kupanda kwa riba miongoni
mwa watumiaji wa huduma za kibenki, hivyo kupunguza nia ya kukopa waliyonayo
wateja wetu na kuathiri mzungunko wetu wa fedha,” alisema Dk. Kimei.
Aliwataka
wadau hao, hasa wanasiasa, waguswe kwa namna moja ama nyingine na ukuaji huo wa
riba kwa Mtanzania wa kawaida ambao unaathiri harakati za maendeleo, na kwamba waelekeze
nguvu zao katika hilo ili kupunguza ukali wa maisha na kuleta maendeleo ya mtu
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment