Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Wakili wa Kujitegemea, Elias Nawera (katikati), akizungumza na wanachama hicho na viongozi mbalimbali wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Kawe Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kawe, Athumani Athumani na Katibu wa CCM wa kata hiyo, Said Kheri.
Makada wa CCM wa Kata ya Kawe wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, Elias Nawera, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Kawe katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwa tiketi ya chama chake.
Akitangaza nia yake mbele ya wanachama na viongozi wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Nawera ambaye ni Wakili wa kujitegemea alisema anayo nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.
Alisema anaamini kuwa anatosha kuliongoza jimbo hilo kwakuwa amekuwa kada kwa muda mrefu na kwamba wakati wa kuwania nafasi hiyo ukifika atakuwa miongoni mwa watakaojitokeza kuchukua fomu ndani ya chama kwa lengo la kugombea kuchaguliwa ili kuwa miongoni mwa wawania ubunge jimboni humo.
"Nataka kulirudisha jimbo ili mikononi mwa Chama cha mapinduzi, hivyo ndugu zangu nimesimama mbele yenu kutangaza nia yangu ya dhati ya kutaka kuwania jimbo ili pale muda utakapofika na mimi nitakuwa miongoni wa nitakaoomba ridhaa kwa chama changu"
"Ndugu zangu nitaomba ushirikiano wenu pale muda utakapofika na kwa pamoja tuhakikishe kuwa jimbo hili linarejea CCM kwa ushindi wa kishindo"alisema Nawera.
Kwa upande wake Meneja Kampeni wake Harold Maruma alisema kwamba anaamini kuwa wakati wa mchakato wa kugombea ndani ya chama utakapofika, Nawera atakuwa miongoni mwa watakaoomba ridhaa ya kuwa mgombea kwa tiketi ya chama hicho.
Alisema kwamba nia ni moja kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi wa kishindo na kwamba kwasasa kinachofanyika ni kuweka nia ukizingatia kuwa jimbo hilo linaongozwa na upinzani hivyo kwa CCM linahesabika kama lipo wazi. (Imeandaliwa na mtandao wa http:www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment