Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya
Shirikisho uwanja wa Karume.
Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:
CLUB LICENCING (Leseni za vilabu)
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi
Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu
wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu
ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu
ifikapo msimu wa 2015/16.
KOMPYUTA
- Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao
uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa
na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka
kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi,
Manyara, Njombe na Simiyu.
MFUKO
WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika
katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba
kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.
Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa
tume hiyo
(i)Tido Mhando - Mwenyekiti,
(ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti
(iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,
(iv)Beatrice Singano - mjumbe,
(v)Joseph Kahama - mjumbe
(vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.
Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo.
AJIRA
Kamati
ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji
mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015.
Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano TFF.
TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.
Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.
TIMU ZA TAIFA
Kamati
ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais
wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi
wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya
Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.
Baada
ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa,
Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake
utasitishwa mara moja.
Maamuzi
haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na
michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.
Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment