Shirika la Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), litaendesha kambi za
upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Tanga.
Lengo la kambi hizi ni
kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama
wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga
tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha
ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi hili litakaloanzia
mkoani Tanga.
Linatarajiwa kwenda Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.Zoezi
litaanza viwanja vya Tangamano kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili
asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma
mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;
- Upimaji wa Shinikizo la damu
- Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
- Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Uzito)
- · Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
- · Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
- · Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.
Huduma zote hizi
zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na
kuwahimiza wakazi wa Tanga kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI
Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji
wadogo, Wavuvi, Ushirika wa Bodaboda ,
Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme
ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia
nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja
na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa Tanga wanakumbushwa
na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao
Bure.
NSSF
INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Meneja wa Mafao ya Matibabu (SHIB) Dk.Ali Mtulia akizungumza
na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali juu ya lengo la kambi ya upimaji
Afya kwa wakazi wa Tanga ambayo inaendelea Mkoani Tanga kwenye Viwanja vya
Tangamano.
Daktari Mtulia (kulia ) na Dk.Limu (kushoto) wakipima uzito na
Urefu wa Mkazi wa Tanga ili kuweza kujua na kumshauri juu ya uwiano wa Urefu na
Uzito wake.
Daktari bingwa wa Siku nyingi Dk. Ali Mzige akimshauri mkazi
wa Tanga juu ya afya yake na lishe bora.
Afisa Matekelezo mkoa wa Tanga, akimuandikisha mmoja wa
wakazi wa Mkoa wa Tanga aliyepimwa Afya na kuamua kujiandikisha kwa hiari na
Mfuko wa NSSF ili aweze jipatia matibabu bure.
Wakazi wa Tanga wakipewa Elimu ya pamoja kabla hawajaamua
kupima kwa Hiari Virusi vya Ukimwi katika zoezi la upimaji afya bure
linaloendeshwa na NSSF.
Wakazi wa Mkoa wa Tanga waliokuja kupima Afya zao kwa
Hiari wakisubiri kuwaona madaktari wa NSSF katika viwanja vya Tangamano.
No comments:
Post a Comment