Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anasema amerejea nchini
humo, huku Naibu Kiongozi wa Mapinduzi akikiri kuwa jaribio la kumuangusha
Nkurunziza limeshindwa. Umoja wa Mataifa umetaka kurejeshwa haraka utawala wa sheria.
Mshauri Mwandamizi wa mawasiliano wa Rais Willy Nyamwitwe,
alisema Nkurunziza amerejea nchini humo, lakini hakutoa maelezo zaidi kwa kile
alichosema ni sababu za kiusalama.
Nkurunziza alikuwa nchi jirani ya Tanzania
kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda siku ya Jumanatano wakati mapinduzi
yalipotangazwa na Jenerali Godefroid Niyombere, na kufunika wiki kadhaa za
maandamano dhidi ya jaribio la rais kutafuta muhula wa tatu.
Taarifa za kurejea kwa rais Nkurunziza hazikuweza
kuthibitishwa na duru huru hata hivyo, na uwepo wake umeendelea kuwa
kitendawili usiku wa Alhamisi. Lakini tangazo kwamba amerudi lilifuatia haraka
na kukiri kwa naibu kiongozi wa mapinduzi Cyrille Ndayirukiye kwamba mapinduzi
hayo yameshindwa. Ndayikuriye aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP,
kuwa binafsi anatambua kuwa vuguvu lao limeshindwa.
Waandamanaji
wanaompinga Nkurunziza wakishangalia baada ya kutangazwa kwa mapinduzi.
Waandamanaji wanaompinga Nkurunziza wakishangalia baada ya
kutangazwa kwa mapinduzi.
Watiifu wadhibiti vituo muhimu
Mapema Alhamis, wanajeshi watiifu kwa rais walisema
walizuwia mashambulizi mawili makubwa yaliyofanywa na wapinzani katika
mapambano makali ya kudhibiti kituo chenye umuhimu wa kimkakati cha redio ya
taifa. Miili ya wanajeshi watatu ilionekana ikiwa imelala mitaani karibu na
eneo la mapigano hayo, ishara ya kwanza ya maafa katika kadhia hiyo ya
mapinduzi. Kufikia mchana, mkurugenzi wa kituo hicho Jerome Nkokirantevye
alisema wanajeshi watiifu ndiyo walikuwa wanakidhibiti kituo hicho.
Afisa mwanadamizi wa polisi alithibitisha taarifa hizo na
kusema jana jioni kuwa wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi walisambaratika
baada ya mashambulizi yao dhidi ya Televisheni ya taifa RTNB na jengo la redio
katika mji mkuu kukandamizwa. Alisema baadhi ya waasi tayari wamejisalimisha na
wengine walikimbia.
Tangazo la mapinduzi la Jumatano lilisababisha ukosoaji
kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na kuibua hofu ya kurejea katika vurugu
kubwa katika taifa hilo maskini, ambalo bado linaedelea kuhisi athari za vita
vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 vilivyomalizika mwaka 2006, na kugharimu
maisha ya maelfu ya Warundi.
Kibonzo hicho
kilichorwa na Said Michael kutoka Tanzania, kuelekea mkutano wa kilele wa
kujadili mgogoro wa Burundi.
Kibonzo hicho kilichorwa na Said Michael kutoka Tanzania,
kuelekea mkutano wa kilele wa kujadili mgogoro wa Burundi.
Baraza la Usalama laonya.
Marekani ilisisitiza Alhamis kuwa Nkurunziza ndiye rasi
halali wa Burundi bado. Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana
katika kikao cha dharura siku ya Alhamis, lililaani jaribio hilo la mapinduzi,
na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria na kufanyika kwa uchaguzi kwa
kuzingatia makubaliano ya Arusha.
Katika taarifa iliyosomwa na Raimonda Murmokaite, balozi wa
Lithuania katika Umoja wa Umoja wa Mataifa, na rais wa barala hilo kwa mwezi wa
Mei, baraza hilo lenye wanachama 15 lilieza utayarifu wake kuchukulia hatua
vitendo vya vurugu nchini Burundi vinavyotishia amani na usalama.
"Wanachama wa baraza la usalama wamelaani machafuko
nchini Burundi na hasa wamewalaani wanaochochea vurugu za aina yoyote dhidi ya
raia, na wale wanaotaka kutwaa madaraka kwa njia zisizohalali," alisema
Murmokaite.
"Wanachama wa baraza la usalama wametoa wito kwa pande
zote kutotumia vurugu na kutoa kipaumbele kwa amani na usalama. Baraza pia
limerejelea uungaji wake mkono wa juhudi la mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa
Said Djinnit, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki."
Wakimbizi wa Burundi
waliowasili nchini Tanzania kufuatia machafuko yanayoendelea nchini mwao.
Wakimbizi wa Burundi waliowasili nchini Tanzania kufuatia
machafuko yanayoendelea nchini mwao.
Maelf wakimbilia nchi jirani Katika taarifa iliyotangazwa kupitia redioni, rais
Nkurunziza alisema analilaani kundi la waliokula njama, na kuwashukuru
wanajeshi wanaorejesha utengamano, na kwamba anawasamehe wanajeshi wanaoamua
kujisalimisha. Umoja wa Mataifa unasema zaidi Warundi 70,000 wamekimbilia nchi
jirani, na kuivuruga kanda hiyo yenye historia ya mapigano ya kikabila.
Wapinzani wanasema jaribio la rais kugombea muhula wa tatu
linakiuka katiba na makubaliano ya amani yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa
wenyewe. Hukumu ya mahakama ya katiba hata hivyo, ilisema rais anaweza kusimama
tena, ikibainisha kuwa muhula wake wa kwanza, alipochaguliwa na bunge badala ya
kura ya wananchi, haukuhesabiwa. Lakini wakosaoji wanasema mahakama hiyo ina
upendeleo.
Chanjo cha habari DW.
Chanjo cha habari DW.
No comments:
Post a Comment