NA
ELIZABETH JOHN
BAADA ya kugombana na mkewe, msanii wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Nurdin Bilal ‘Shetta’ amesema kuwa, endapo kama mkewe atarudi
nyumbani amemuandalia zawadi ya gari aina ya Mark X.
Mke wa Shetta (mama Kaila), aliondoka nyumbani kwake baada
ya msanii huyo kudaiwa kulala chumba kimoja na msanii wa filamu nchini, Rose
Ndauka mjini Morogoro walipokwenda kwenye msiba wa aliyekuwa muasisi wa Top Top
Connection, marehemu Abdul Bonge.
Akihojiwa na Clouds FM, Shetta alisema kuwa, mkewe hataki
kabisa kumuelewa kuhusu suala hilo na sasa hivi anadai taraka akisema kwamba
uhusiano wao ubaki kwa kumhudumia mtoto tu.
“Yani hataki kabisa kunielewa, nafikiri kuna mtu ambaye
anampa maneno ya uongo lakini kiukweli kabisa mke wangu bado nampenda sana tu
sijui kwa nini hataki kunielewa maana nimefanya vitu vingi kanielewa na endapo
akirudi nimeandalia gari la kutembelea yeye pamoja na mtoto,” alisema.
Shetta kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Shikorobo’
ambayo amemshirikisha nyota kutoka Nigeria, KCEE.
No comments:
Post a Comment