NA ELIZABETH JOHN
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' amesema
kuwa hakuweza kuhudhuria kwenye ‘Zari All White Party’, kwa sababu hakualikwa.
'Party' hiyo ambayo ilifanyika Ijumaa iliyopita, iliandaliwa na mfalme wa
muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul 'diamond Platinumz' ambaye ni rafiki
wa Dimpoz.
Akihojiwa na Redio 5 ya jijini Arusha, Dimpoz alisema kuwa, kunyimwa
mwaliko wa kuhudhuria 'party' hiyo hakumaanishi kuwa ana tatizo na Diamond.
“I am not invited', sina tatizo na Diamond, hajawahi kunikosea, kikubwa ni
kwamba amekuwa ni mfano kwa wasanii wachanga kwasababu hata mimi nimemkuta
kwenye muziki na ni mmoja wa wanamuziki ambao walikuwa wananivuta hata mimi
kuwa achana na mambo ya bendi na kuwa 'solo artist," alisema.
Dimpoz kwasasa anatamba na ngoma yake ya 'Wanjera' ambayo imeanza kufanya
vizuri Kimataifa.
No comments:
Post a Comment