Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana kabla ya safari ya kuelekea Afrika Kusini katika mashindano ya COSAFA yanayotarajiwa kuanza Mei 17 hadi 30. (Picha na Francis Dande)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.
Michuano
ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015
katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West
Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika
huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
Taifa
Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa
usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5
usiku.
Mara
baada ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka
Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub
wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi
kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazoezi
chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na
kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa
ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
Msafara
wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF,
Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu
inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya
jiji la Rusterburg.
Kesho
siku ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ni muda wa
mapumziko, waandishi wa habari mnakaribishwa katika kambi ya timu ya
Taifa iliyopo Tansoma Hotel kuweza kuongea na wachezaji, kocha mkuu na
daktari wa timu kabla ya kuanza safari jioni.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
No comments:
Post a Comment