HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2015

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADARASA MATATU NA MADAWATI KATIKA SHULE YA MSINGI TALATALA MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa pamoja na madawati katika Shule ya Msingi ya Talatala iliyopo wilayani humo.Benki ya CRDB ilitoa msaada wa kujenga madarasa matatu pamoja na kununua madawati 60 vikiwa na thamani ya shilingi milioni 60.
 Mkurugenzi  wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa matatu kwa Shule ya Msingi Talatala iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Baadhi ya wazazi wakiwa katika hafla ya kukabidhi madarasa kwa Shule ya Msingi Talatala.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Talatala wakiimba nyimbo.
Mkuu wa Shule ya Talatala, Boniface Jackson akitoa hotuba yake.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kyela, Lugano Mwambaja (kushoto) akiwa na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mbalali, Chibby Chibby (kulia)
 Wazazi na Wanafunzi na wa Shule ya Msingi, Talatala wakimsikiliza mgeni rasmi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala akipongezwa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa baada ya kutoa hotuba yake.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala akicheza muziki na mmoja wa wanafunzi.
Madarasa yaliyojengwa na Benki ya CRDB.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala (wa nne kushoto), akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa matatu yaliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB kwa Shule ya Msingi ya Talatala iliyopo wilayani humo. Benki hiyo pia ilikabidhi madawati 60 kwa shule hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa, Mkuu wa Shule, Boniface Jackson, Mkurugenzi  wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa tatu kushoto) na Meneja wa Tawi la Kyela, Lugano Mwambaja (wa pili kushoto).

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala (kulia) akiwa amekaa katika moja ya madawati yaliyokabidhiwa na benki ya CRDB kama msaada katika Shule ya Msingi Talatala iliyopo wilayani Kyela. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kyela, Lugano Mwambaja. Benki ya CRDB ilikabidhi madarasa matatu pamoja na madawati 60.
  Mkurugenzi  wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akicheza na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Talatala.
Mkurugenzi  wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akipokea kwa furaha zawadi ya mkeka kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Talatala Kati, Agneta Mwaisaka mara baada ya kukabidhi madarasa matatu pamoja na madawati 60 katika Shule ya Msingi Talatala iliyopo wilayani Kyela juzi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala.

No comments:

Post a Comment

Pages