HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 10, 2015

BOA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA UENDELEZAJI ARDHI YA AVIC

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Masia Mushi, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, kuhusu mradi mkubwa wa mikopo nafuu ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, zilizopo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao utawanufaisha watanzania hususani wateja wa benki ya BOA, ambao ulisainiwa rasmi leo. Katikati ni Naibu Meneja Mkuu wa AVIC, Liu Dexiang na kushoto ni Mwanasheria wa kampuni hiyo, Li Jiayin.
 Viongozi wa Bank of Africa (BOA) kwa pamoja na viongozi wa Kampuni ya Kimatiafa ya Uendelezaji wa Ardhi (AVIC), wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya mikopo nafuu uuzaji wa nyumba zilizojengwa ka kampuni hiyo, zilizopo eneo la Somangira, Kigamboni, Dar es Salaam. Hafla ya kusaini mktaba huo ilifanyika leo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakisaini mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakibadilishana hati za mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusaini leo, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanasheria wa BOA, Patrick Malewo na kushoto ni Mwansheria wa AVIC, Li Jiayin.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Masia Mushi, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mkataba wa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, wa mikopo nafuu ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao utawanufaisha watanzania hususani wateja wa benki ya BOA, kabla ya kusainiwa mkataba huo rasmi leo. Kushoto kwake ni Mwanasheria wa benki hiyo, Patrick Malewo.

No comments:

Post a Comment

Pages