NA ZAWADI CHOGOGWE
HOSPITALI ya CCBRT iliopo Msasani jijini Dar es Salaam
imefungua kiwanja cha michezo tofauti tofauti
ya watoto hospitalini hapo.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kiwanja hicho, Mwenyekiti wa kamati ya
mashindano ya mbio za mbuzi ‘Dar
es Salaam Charity Goat Races’, Karen Stanley alisema
kitasaidia katika kuhamasisha afya ya watoto walioko wodini kwa kucheza,kupumzika na kuweza kujumuika na
watoto wengine.
Alisema kuwa kuwa CCBRT ilitambua kuna umuhimu mkubwa wa
kuboresha kiwanja cha michezo cha watoto kilichokuwa kimechakaa kwa kujenga
upya na kuongeza ubora wa kivuli cha kupumzika.
Alisema michezo ina sehemu kubwa katika ratiba za
matibabu ya watoto waliopo hospitalini
haswa walioko kwa muda mrefu kwa lengo la kuwaondolea mawazo na kuwafanya wawe
sehemu ya jamii iliyona afya bora.
“Kulazwa hospitalini si tukio la kawaida na mara nyingi
husababisha msongo kwa watoto na familia zao, hivyo kwa kufunguliwa kwa kiwanja
hiki kitawajenga watoto kisaikolojia." Alisema na kuongeza kuwa
“Kuwepo kwa eneo hili ambalo watoto wanaweza kucheza,pia
husaidia kuwapa muonekano mzuri juu ya muda wao
kwa muda wote watakaokuwa hapa hospitalini”
Alisema kwa kupata uwanja huo utawafanya watoto kuweza kumudu
baadhi ya matibabu yakiwemo ya upasuaji na magonjwa mengine wakati wakiwa hospitalini.
Stanley alisema kuwa uwanja huo ulianza kujengwa Desemba
mwaka jana na kukamilika rasmi mwezi juni mwaka huu kwa udhamini wa mashirika manne ya Irish Aid, Dar
es Salaam Goat Races, Corona Society of Tanzania na Familia ya Wetzel.
No comments:
Post a Comment