NA ZAWADI CHOGOGWE
ASASI isiyokuwa ya kiserikali
ya Women In Society (WOISO), katika kuadhimisha siku ya Watoto Duniani Juni 6
mwaka huu inatarajia kuzindua
Albamu zenye ujumbe wa watoto
katika uzinduzi utakaofanyika katika viwanja vya Kijitonyama.
Sambamba na uzinduzi huo, wenye
kauli mbiu ya ‘Thamani Yetu Leo’kutakuwa
na burudani mbalimbli zikiwemo ngoma za
asili,sarakasi na maigizo.
Akizunguza na wanahabari jijini
Dar es Salaam leo ,Mwenyekiti wa nidhamu wa asasi hiyo, Zenais Mtebe,alisema
kuwa watakaohudhuria katika uzinduzi huo wataelimika na ujumbe utakaotolewa
katika uzinduzi wa albamu hiyo na kupata burudani ya pekee kutoka kwa wasanii
mbalimba wazoefu na chupukizi.
Alisema mbali na burudani
hizo kutakuwa na elimu namna ya kuwasaidia watoto ambao wanafanyiwa vitendo vya
ukatili.
Aliongeza kuwa uzinduzi huo
utatumika kusambaza machapisho mbalimbali ya kuelimisha jamii ambapo wataanzia
na mikoa ya Pwani ,Tanga,Morogoro, Mbeya
na Mwanza.
Mtebe alisema Mgeni rasmi
katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Afya na Uzazi na Malezi Bora (UMATI),
Lulu Mwanakilala.
Naye Mwenyekiti wa Bodi , Juliana
Madeleke, alitoa wito kwa wazazi kuwapeleka kwa wingi watoto katika uzinduzi
huo kwa lengo la kujifunza elimu itakayotolewa katika uzinduzi wa albamu hiyo.
“Jamii ya sasa imekua ikipoteza
maadili ya kitanzania na badala yake imewasahau watoto katika misingi ya
kupenda zaidi utandawazi ambao umeharibu misingi imara ya jamii kwa kutokana
mazingira ya huko, hivyo wazazi walateni watoto wajifunze maadili mema na
nyimbo zenye ujumbe mzuri kwa taifa la Tanzania” alisema.
This is Nice and Wonderful!!
ReplyDelete