HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2015

DIAMOND KUIBEBA VIDEO YA KIMADOIDO


NA ELIZABETH JOHN

MFALME wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye atakayegharamia gharama za kutengeneza video ya ngoma ya ‘Cheza Kimadoido’ iliyoimbwa na kundi la Yamoto lenye maskani yake Temeke, jijini Dar es Salaam.

Video hiyo itatengenezwa nchini Afrika Kusini katika kampuni ya Godfather Production chini ya mtayarishaji mahiri Godfather.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kundi hili, Said Fela ‘Mkubwa Fela’, msanii huyo ameahidi kufanya hivyo kutokana na kuyakubali mashairi ya vijana wangu ealiyoimba katika ngoma hiyo.

“Diamond ni mteja wa Yamoto, yeye kama msanii ameukubali wimbo huo na kuamua kutoa zawadi kwa wadogo zake, binafsi nimefurahishwa na hilo kwa sababu ameonesha upendo kutokana na kazi wanayoifanya vijana wangu,” alisema Mkubwa Fela.

Wasanii ambao wanatamba katika kundi hilo ni Maromboso, Aslay, Beka One na Enock Bella huku wakitamba na ngoma zao za ‘Yamoto’, ‘Niseme’, ‘Itakupwelepweta’, ‘Nitajuta’, ‘Nikupeti peti’ na nyinginezo.


No comments:

Post a Comment

Pages