HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 01, 2015

JAJI ANTONY BAHATI KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI

 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Jaji mstaafu, Antony Bahati nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Mazishi ya jaji Bahati yatafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya waombolezaji.
 Ndugu na jamaa wakiwa nyumbani kwa marehemu jaji mstaafu Antony Bahati.
 Waombolezaji wakiwasili nyumbani kwa marehemu.
 Jaji Antony Bahati enzi za uhai wake.
 Waombolezaji wakiweka sahihi kitabu cha maombolezo.
Mwili wa Jaji mstaafu Antony Bahati ukiwasili nyumba kwake Oysterbay ambapo mazishi yatafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. 
Mwili wa Jaji mstaafu Antony Bahati ukiwasili nyumba kwake Oysterbay ambapo mazishi yatafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. 
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani.
 Watoto wa marehemu wakiwa na huzuni mara baada ya mwili kuwasili nyumbani.
 Mwili ukiwa umehifadhiwa nyumbani.
Mtoto wa marehemu Thomas Bahati (kushoto) akiwa na akiwa na huzuni baada ya mwili kuwasili nyumbani.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Marehemu Jaji mstaafu Antony Bahati alizaliwa tarehe 13.12. 1940 katika kijiji cha Butundwe wilayani Geita Mkoa wa Geita, marehemu ni mtotto wa pili katikafamilia ya marehemumzee ThomasMaziku Nabiji na Aurelia Mganda. Alipatizwa na Aprili 21 1941 Kome Geita, aidha alipata Komunio na Kipaimara mwaka 1952 Kome Geita.  Alisoma katika Shule ya Msingi Buhingo kuanzia mwaka 1948-1951.

Alijiunga na Nyegezi Seminari kwa darasa la tano hadi la kumi na nne na tangu mwaka 1952 hadi mwaka 1962  Marehemu Jaji mstaafu Antony Bahati alijiunga na masomo ya falsafa katika seminari kuu ya Kipalapala na baadae kufundisha katika seminari ya Nyegezi tangu mwaka 1962 hadi 1965.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1965, ambapo alihitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) Mwaka 1969.

Marehemu Jaji Antony Bahati amehudhuria kozi fupi katika nchi mbalimbali duniani, kama uzuiaji wa uhalifu, utatuzi wa migogoro, urekebishaji wa sheria, nk.

Marehemu alifunga ndoa na Laurencia Michael (ambaye ni marehemu) Desemba 26 1963 Mwanza Cathedra Bugando. Katika uhai wake na mke wake wamebahatika kupata watoto nane wa kike saba na wa kiume mmoja na wamebahatika kupata wajukuu kumi na nne.

Marehemu Jaji Antony Bahati aliajiriwa serikalini Aprili 12-1969 kama Hakimu Mkazi Daraja la 111 na kuthibitishwa kazini Septemba 7-1972. Amepanda vyeo mbalimbali kuanzia Hakimu Mkazi Daraja la 11, Hakimu Mkazi Daraja la Kwanza na Hakimu Mkuu Desemba mosi 1979. Aidha alipata uteuzi mbalimbali kama ifuatavyo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Rufani (1981), Kaimu Jaji wa Mahakama Kuu (1982-1983), Jaji wa Mahakama Kuu Juni 24-1983, Mwenyekiti wa Mahakama ya Kazi 1993-1996 na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Novemba 30-1996 hadi Novemba 2006.

Marehemu Jaji (Antony Bahati amefanya kazi sehemu mbalimbali nchini ambapo kituo chake cha kwanza kupangiwa kazi kilikuwa Musoma tarehe 15-5-1969 baada ya hapo alihamishiwa Tukuyu, Tabora, Bukoba, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.

Marehemu Jaji Antony Bahati alistaafu utumishi katika nafasi ya Jaji wa Mahakama Kuu tarehe 13-12- 2000.
Marehemu alianza kupata matatizo ya kiafya mwaka 1995 ambapo aligundulika kuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo lililosababisha apelekwe nchini Afrika Kusini ili apate matibabu zaidi. 

Baada ya matibabu yake nchini Afrika Kusini ambayo yalikuwa ni ya mafanikio makubwa, alirudi nchini na kuendelea na majukumu yake aliyokuwa amepewa na serikali. Hata hivyo, hali yake tatizola ugonjwa wa moyo ilijirudia tena na ilibidi apelekwe katika Hospitali ya Apollo, Chennai nchini India mwaka 2009 na 2011 ambapo alitibiwa na kupata nafuu. Hali ya tatizo la kiafya kwa marehemu iliendelea kujitokeza katika maisha yake ya ustaafu ambapo alikuwa akilazwa mara kwa mara katika hospitali ya Agakhan na kupata matibabu na baadae kupata nafuu.

Hata hivyo pamoja na juhudi kubwa za madaktari kuokoa maisha yake ilipofika tarehe 28 Mei, 2015 saa 5 usiku marehemu alifariki dunia. Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani, Amen.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe, AMEN.

No comments:

Post a Comment

Pages