Mheshimiwa Zitto Kabwe amefunguka
katika ukurasa wake wa Facebook na kumponda mbunge wa Bumbuli, Mheshimiwa
January Makamba, kutokana na hotuba yake aliyoisoma jana katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati akitangaza nia ya kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015.
Ujumbe aliouandika
Mheshimiwa Zitto Kabwe
January alijieleza kwa ufasaha
zaidi kuliko wote. ‘Content’ kawazidi wenzake wote. Hata hivyo ameshindwa
kabisa kutamka miiko ya viongozi. Bila miiko, yote aliyoyataja hayatafanyika,
maana ufisadi utatamalaki. Unaweza kuondoa rushwa kwa sheria. Lakini huwezi
kuondoa ufisadi bila Miiko ya Viongozi. Sijui kwanini kijana mwenzangu kaona
aibu japo kutaja neno miiko. Uchaguzi wa mwaka huu umeegemezwa kwenye kurudi
kwenye misingi iliyoasisi taifa.
Nimeridhika sana na ‘content’ na ‘context’.
Sikubaliani na mwono. January Makamba anaiona Tanzania ya kibepari. Nadhani
inabidi kufumua uchumi wa kibepari na kujenga uchumi wa kijamaa. I would love
to debate him on the kind of the nation we shall rebuild. Kila la heri rafiki
yangu.
Maoni ya
watu waliyoyatoa...
Faraja MG
Ubepari ndo wenyewe. Ujamaa
tulishauzika. Huwezi endelea na ujamaa.
Jimy Macha
Katumia sana shule kwenye kujieleza
kuliko uhalisia...
Joseph PJP
Ingekuwa tunawapima wagombea kwa kujieleza basi nchi hii MC wa sherehe wangefaa kuwa marais wetu! Na
watunga hotuba kama yeye, hiyo ilikuwa ajira yake kuandika hotuba.
Kimsingi
January ni uzao wa huo mfumo anaoulalamikia kuwa atauletea Mabadiliko! Baba yake amekuwa kwenye ‘same system’ iliyofeli, anayoilalamikia kuwa imefeli! For 50 years, genetically he has proved us right kuwa hana jipya sawa
na wazazi wake walivyofeli na yeye amefeli! refer to simcard tax na tozo ghali za simu, MB 8, hayo ni mambo madogo tu
kafeli.
hatujasahau hiyo sheria ya mitandao
aliyokuja nayo ya kuzima moto na sasa haiwezi kufanya kazi. In short ni ngumu
fisi kuzaa swala!
Si mimi, ni kanuni ya genetics!
David
Mssika
January Y. Makamba did well. Maybe
hizo kasoro ziwe ni challenge kwake. Nimependa ufufuaji wa njia za uchumi na
mikakati ya kuongeza/kupata fedha from within!
Hii itapunguza dependency syndrome!
Kitu nimekosa kwa wote ni usalama wa raia na mali zao, usalama wa nchi na namna
ya kuboresha demokrasia.
Albert
Kamwela
Nina shaka na utekelezaji. Maneno
yanakuwa mengi kuliko utekelezaji.
Goodluck
Andrew Msaky
Hivi mradi wa MKURABITA ungeenda
ipasavyo hawa watia nia wangezungumza kitu gani?
Anatuambia ataunda baraza la
mawaziri 18 lenye maadili wakati hiyo sera ilikuwepo kwenye rasimu ya katiba ya
Jaji Warioba na ndiyo hiyo CCM wameipiga vita bungeni akiwemo, sasa leo
anatuambia kitu gani? Naona kama anakosoa yaliyofanywa kipindi cha awamu ya nne
na yeye alikuwa na uwezo wa kushauri kama naibu waziri mambo yakaenda sawa.
Manywele
Omary
Chui katika ngozi ya kondoo..
Nadharia na vitendo ndo tofauti kubwa kwa viongozi wa CCM, so far me naona
Mwigulu Nchemba ndo yupo na real inner spirit ya mabadiliko.
Lyaruu
Engelbert John
Ni mkusanyiko wa yale yale!! Kweli
hatujapata jibu la changamoto zetu. Hawa walikuwa na rais mbona haya
wanayoongea hawakufanya katika wizara zao? Au rais hakuwa na utashi! Tujiulize.
No comments:
Post a Comment