Wachezaji wa Stars wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa Benki ya Biashara ya
Ethiopia jana ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Misri. (Picha na TFF)
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro kimeendelea kujifua katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia eneo la CMC asubuhi na jioni katika uwanja wa Taifa wa Addis Ababa.
Golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Aishi Manula akiwa katika mazoezi ya
kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Misri kwenye Uwanja wa Benki ya Biashara ya
Ethiopia.
Golikipa wa Stars, Mwadini Ally.Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro kimeendelea kujifua katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia eneo la CMC asubuhi na jioni katika uwanja wa Taifa wa Addis Ababa.
Stars
ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa imekua ikijifua mara mbili kwa
siku, kuhakikisha wachezaji wanakua vizuri kuelekea katika mchezo dhidi
ya timu ya Taifa Misri mwishoni mwa wiki hii jijini Alexandria.
Hali
ya kambi kiujumla ni nzuri, wachezaji wote ni wazima, wakiwa wenye ari,
na morali ya hali ya juu katika maandalizi ya mchezo huo wa kuwania
kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars mholanzi, Mart Nooij amekuwa akiwafundisha vijana
wake mbinu mbali mbali kuelekea kwenye mechi dhidi ya Misri, kuanzia
sehemu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji kuhakikisha wanakua fit katika
mchezo unaowakabili.
Ikiwa
ni siku ya nne tangu Taifa Stars kuanza mazoezi yake jijini Addis
Ababa, kocha Nooij amesema anashukuru vijana wake wanamuelewa vizuri
anachowaelekeza, sasa timu inacheza mpira wa kasi na pasi za haraka
haraka, vijana wamechangamka na morali ni ya hali ya juu kambini
kuelekea kwenye mchezo unaowakabili.
Hali
ya nidhamu kambini ni ya hali ya juu, wachezaji waanatambua umuhimu wa
mchezo huo, na kikubwa wameahidi kupambana kusaka matokeo mazuri katika
mchezo dhidi ya Misri.
“Katika
mpira hakuna kinachoshindikana, sie tumejiandaa vizuri, naamini
tutakapofika Misri tutafanya vizuri na kuwapa furaha watanzania, kikubwa
watuombee kwa mwenyezi mungu, tuwe wazima mpaka siku ya mchezo, naamini
tutafanya vizuri” alisema Nadri.
Stars
inatarajiwa kuelekea jijini Cairo siku ya ijumaa, kisha kuunganisha
katika jiji la Alexandria tayari kwa mchezo dhidi ya Misri utakaochezwa
katika uwanja wa Boeg El Arab siku ya jumapili Juni 14, 2015.
NB: Picha za mazoezi ya Taifa Stars zimeambatanishwa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment