Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na wana jogging wa Kata ya Msasani Dar es Salaam leo asubuhi kwenye hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging Club.
Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti (kulia), akihutubia katika hafla hiyo.
DC Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanamsasani Jogging Club.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoki Paul Makonda akiondoka baada ya kuhudhuria hafla hiyo na kuhutubia.
Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amewataka vijana waliopo katika shirikisho la umoja wa Jogging wa Kata ya Msasani kuunda umoja ambao utawasaidia kupata fursa mbalimbali.
Makonda alitoa mwito huo wakati akizungumza na wana jogging waliopo kwenye shirikisho hilo kutoka katika kata hiyo wakati wa hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging.
"Naomba fanyeni mchakato wa kuanzisha Kamati ya Uchumi na Mipango na muuanzishe umoja wenu uliosajiliwa, utawasaidia kupata mikopo na sisi kama serikali tutawapa kazi kama za kukusanya takataka, ulinzi na nyingine nyingi" alisema Makonda.
Alisema Manispaa ya Kinondoni imetenga zaidi ya sh. bilioni 2 kwa ajili ya vijana na wanawake fedha zitakazo tolewa kupitia makundi mbalimbali yaliyosajiliwa.
Alisema fedha hizo zipo kwa ajili ya shughuli mbalimbali na kuwa kwa awamu ya kwanza zitatolewa sh.milioni 100.
Katika kusaidia mchakato wa kuanzisha umoja huo, Makonda alitoa sh. milioni 1 na Diwani wa Kata hiyo, Christina Kirigiti alitoa sh. 300,000 papo hapo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
No comments:
Post a Comment