Mashabiki na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF)
wakinyanyua juu mikono na picha za Maalim Seif Sharif Hamad kuonyesha kumuunga
mkono katika nafasi ya kuwania urais wa Zanzibar, wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba,
akimtangaza Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto),
kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika mkutano
wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti, mjini Zanzibar. (Na Mpiga Picha
Wetu).
Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye ameteuliwa na chama chake
hicho kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika Kibanda Maiti, Mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment