HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2015

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA

 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
 Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo.
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka  sehemu na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao.
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
 Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
 Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
 Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima

No comments:

Post a Comment

Pages