‘Tembo hashindwi na Mkonga wake’
Na Bryceson Mathias
WASWAHILI wanasema, ‘Tembo hashindwi na Mkonga wake’; Hivyo, ni Imani yangu, Wandishi wa nchi hii, hawawezi kushindwaa, ‘Kuwahabarisha Watanzania kupitia, Tasnia ya Habari na Vyombo Vyao’, ili kuweka peupe, Maovu yanayoikabili Tanzania.
KWA sehemu kubwa, Imani na Mategemeo ya Wananchi Tanzania, ni kwa Wandishi wa habari kama Mhimimili wa Nne (Watchdogs) wa kuwakomboa, kwamba ndio, wanatarajiwa wajibu Maswali na Kiu ya Kero zao, hivyo Wandishi hawatakiwi kufanya Masihala, wawajibike.
Tumejifunza huko nyuma, Tasnia ya habari, mara kadhaa imejaribu kujibu Kilio cha Wananchi, has pale Wananchi waliporejeshewa Haki walizodhulumiwa, na ifahamike, Haki hizo zilirejeshewa sababu ya Kelele na Kazi kubwa iliyofanywa na Wandishi na Vyombo vya Habari.
Mwaka huu, Oktoba 25, Wananchi watapiga Kura kuchagua Viongozi, Madiwani, Wabunge na Rais, watakaoongoza Taifa hili, kwa miaka Mitano Ijayo, na ndiyo maana Watia Nia wa kugombea Urais, wameanza na wanaendelea kutia Nia, na Mchakato wa kuchukua Fomu.
Mbali ya kutia na kuchukua Fomu, zipo Kauli wanazotoa, ambazo Wandishi na Tasnia ya Habari, lazima tuwe makini na rejea, tusipuuze na kudharau Kauli hizo, kwa sababu kwa sababu namna moja au nyingine, wanajibu Kiu, Kilio, Kero na Matakwa ya Walaji wa Habari (Wasomaji).
Ukiniuliza kwa nini nataka Kauli zao zisipuuzwe, ni kwa sababu, katika Kauli hizo, baadhi yao wanasema Uongo, ambazo hawakufanya wao, wasiseme, jambo fulani amefanya yeye, wakati aliyefanya ni mwingine, ila anataka kubebe utukufu usio wake, hata walipofanya wananchi.
Ni rai yangu kwa Wandishi, wasiache Ombwe la Maswali Magumu ya Wananchi dhidi ya kile ambacho wananchi wangependa kulishwa kama walaji wa habari mpya na za mwendelezo zinazoibuliwa na Kauli zao.
Kutokana na Watangaza Nia kuomba wachaguliwe Urais wa nchi hii, wananchi wanayo Maswali dhidi yao, ambapo Tasnia ya habari, ilazimake kuwahoji watangaza Nia watoe Majibu ya tuhuma walizotuhumiwa kwenye maeneo yao ya kazi wakiwa madarakani, .
Kwa Ujumla, Wandishi wanatakiwa wawapatie wananchi majibu ya matamko ya Wagombea. Mfano; tuhuma zilizojitokeza kabla ya Safari ya Matumaini, Richmond ya Nani? Dowan’s ya Nani? Na Kama kuna Mtu anasema anatuvusha Ng’ambo, anatumia njia gani? Tuhuma zake Je!
Kama kuna Mtu anasema atatutolea Umaskini; Je watu hao walikuwa wapi kwenye Serikali iliyopita kutoa mawazo ya kuondoa Umaskini? Je umaskini unaondolewa mara baada ya kujinufaisha binafsi unatoka wapi?
Kwa Matamko ya Watangaza Nia; Ni rai yangu, Kauli zilizotolewa na Watia Nia na Wagombea Urais, ningependa Kauli kama ya, Makongoro Nyerere, kwamba nchi hii imezungukwa na Vibaka, ni vyema Wandishi (Macho ya Taifa), Wasiipuuze Kauli ya Nyerere! Watusaidie tujue, Vibaka hao ni Nani?.
Mbali ya Nyerere katika Nia yake, Watuhabarishe, ni kwa namna gani, Vibaka hao walitaka kumpindua Rais, Jakaya Kikwete, katika Uongozi wake wa Chama cha Mapinduzi (CCM)?, Wandishi tunatakiwa tupekue ndani, tujue ukweli na uhalisia wa kile anachotuhabarisha Makongoro, ili tuwahabarishe Wananchi, ukweli huo!.
Nyerere ni Mtoto wa Mwasisi wa Taifa hili, anaposema, ‘turudishieni Chama chetu’! Lazima Wandishi tujiulize, ana maana gani? Pia ni vema tuwe na kumbukumbu, yaani rejea, ambazo kama mgombea alituhumiwa jambo, lazima aulizwe tupate majibu toka, ‘Kinywani mwake’.
Nimalize kwa kusema hivi, mtu anaweza kuniuliza kwa nini nataka Watia Nia na Wagombea Urais, wajibu kile walichotuhumiwa nacho. Uongozi ni kama Mzoga, unakaribisha Nzi, Unakaribisha Fisi, na unakaribisha Mbwa Mwitu, ambao ni Waroho wa Nyama! Hata kama Imeoza!.
Chonde; ‘Wandishi tusiwe kama Maji ya Moto’, ambayo hupoa kutoka kwenye Moto wake, kila muda unapokwenda.
0715-933308
No comments:
Post a Comment