Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana kwa furaha na Waziri mwenzake, Profesa
Mark Mwandosya, wakati walipokutana Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi,
wakiwa kwenye harakati za kusaka wadhamini mkoani humo.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwaaga baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza
kwenye Ofisi ya CCM wilayani Mpanda, jana, wakiomba kumdhamini katika harakati
zake za kuwania kupeperusha bendera ya Chama katika nafasi ya urais. Nyalandu
alikuwa mkoani humo kusaka wadhamini, ambapo mamia walijitokeza.
MKE wa Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Farajam akiwa na mke wa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Asiye na Wizara Maalum), Profesa Mark Mwandosya, wakati
wapokutana Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi, kusaka wadhamini. Nyalandu
na Profesa Mwandosya wote wanawania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera
kuwania urais.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema mbio za kuwania kurithi mikoba ya Rais Jakaya Kikwete zisitumike kuwagawa wanaccm na badala yake ziongeze umoja na mshikamano ndani ya chama.
Amesema hatua
ya kujitokeza kwa viongozi wengi kuutaka urais inadhihirisha ccm ina
hazina kubwa ya viongozi ambayo inapaswa kulindwa kwa maslahi ya taifa.
Amesema miongoni mwa wengi waliojitokeza, lakini nafasi hiyo itakwenda
kwa mwanaccm mmoja ambaye ni lazima aungwe mkono na wote ili kuhakikisha
ccm inashinda.
Nyalandu ambaye ni miongoni mwa makada vijana wenye
nguvu na ushawishi mkubwa kutokana na utendaji kazi wake, aliyasema hayo
jana wakati akizungumza na mamia ya wanaccm waliojitokeza kumdhamini
mkoani mara.
"Ndugu zangu kila siku viongozi wetu wa juu wanasema chama kwanza, mtu baadaye na katika mbio hizi wagombea ni wengi lakini mwisho wa siku kitapata dereva mmoja ambaye ataendesha hili gari na kuwafikisha watanzania safari yao ya maendeleo kwa Amani na usalama" alisema nyalandu.
Alisema mchakato wa urais ndani ya ccm ni demokrasia na
inatekeleza taratibu na kanuni za chama hivyo, mwisho wake lazima wote
tuungane na kuwa kitu kimoja.
Alisema makundi na mgawanyiko ndani ya ccm
usipewe nafasi kwani, unaweza kuleta madhara. Huku akishangiliwa na
mamia ya wanachama, nyalandu alisema adhma yake ni kuwaunganisha
watanzania kuwa kitu kimoja na kuharakisha maendeleo.
Alisema Tanzania
imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo mbuga za wanyama, madini
lakini kubwa ni watu wake ambao ndio rasilimali kubwa. "Niko hapa mara
mahali penye historia ya pekee ya taifa hili, kila mmoja anafahamu na
kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na bana wa taifa. Sasa lazima mema yote
aliyofanya yatumike kuleta mshikamano na umoja kwa taifa hili. Mwalimu
alisema bila ccm madhubuti nchi itayumba, sasa mchakato ukiisha tuungane
na mgombea wa ccm ili tushinde.
Tu ache makundi kwa sababu mungu
alisema ndio hakuna wa kupinga. Rais wa Tanzania atakuwa mmoja na mungu
pekee ndiye anamjua hivyo, tusigombane," alisema.
Nyalandu aliendelea kuwaomba wanaccm kuendelea kuwa na imani naye na kumuunga mkono ktk harakati zake na kwamba, kujitokeza kwao kwa wingi ni ishara kuwa ana vigezo na anatosha kubeba jahazi la ccm.
Alisema amekuwa ndani ya chama, bunge na serikali hivyo amejipima na ana vigezo vya kuongoza taifa.
No comments:
Post a Comment