Baadhi ya wafanyakaz wa CBA Tanzania na Mkombozi wakishangilia uhamasisha timu zao uwanjani.
Mkurugenzi
wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa
Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa mechi ya fainali baina ya timu
iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA
imenyakua ubingwa
Mkurugenzi wa CBA Tanzania Julius Mcharo akiongea na wachezaji baada ya kumalizika mchezo huo
Wacheaji wa CBA Tanzania na Mkombozi wakiwa wamejipanga kukaguliwa kabla ya mchezo kuanza
Wacheji wakionyeshana ubae uwanjani.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya soka ya Benki ya CBA Tanzania imeichapa timu ya Benki ya Mkombozi FC kwa
magoli 3-2 na kufanikiwa kuondoka na kombe la ligi ya mabenki na mifuko ya
hifadhi ya jamii kwa mwaka huu sambamba na kitita cha shilingi milioni moja
taslimu katika fainali zilizofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.Vinara wa mabao waliong’ara katika mchezo huo ni Jessy
Nyambo wa CBA FC David wasongwa wa Mkombozi FC.
Pia timu ya Benki ya Mkombozi ambayo
iliibuka na ushindi wa pili ilijinyakulia kitita cha shilingi laki nane na
kombe.
Akizungumza wakati wa
fainali hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Dar es Salaam Emanuel
Kazimoto, alisema kuwa mashindano hayo ya
taasisi ni muhimu kwa kuwa yanaziunganisha taasisi mbalimbali kuwa na
ushirikiano katika kazi na wafanyakazi kuweza kujenga miili yao kupitia kufanya
mazoezi na aliahidi kuwa watazidi kuunga mkono mashindano ya aina hii na
kuzishauri taasisi hizo kubuni mashindano ya aina mbalimbali yatakayoshirikisha
wafanyakazi wengi zaidi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,Julius Mcharo alisema amefurahishwa na
ushindi ambao vijana wake wamepata na kuongeza kuwa wataendelea kushiriki na
kudhamini michezo mbaimbali kwa kuwa
wanaamini kuwa michezo inaleta mshikamano na kujenga umoja ikiwemo pia
kuimarisha afya.
Meneja Masoko wa Benki ya
Mkombozi Grace Mboya,alipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano hayo na
kusema kuwa kinachotakiwa ni kujiimarisha zaidi ili yazidi kuongezeka ubora kwa
kushirikisha timu za taasisi zote zilizopo katika sekta ya fedha.
Baadhi ya wachezaji wa
timu hizo ambao ni wafanyakazi wa enki hizo wamesema kuwa mashindano hayo
yameweza kuwakutanisha na kuweza kufahamiana zaidi na pia ni moja ya mazoezi ya
kujenga miili yao.Michuano hiyo iliyoanza Mwezi April 2015 na kufunguliwa na
Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba yameshirikisha timu za soka za mabenki na
mashirika ya hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi
wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa
Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa mechi ya fainali baina ya timu
iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA
imenyakua ubingwa
No comments:
Post a Comment