Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita hapa kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.
Aliongeza kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz .
Napenda mtambue hii ni historia katika ukanda huu kuweza kutumia teknojia kufikia wanachama, Sisi ni wakisa sana tunaona mbele!.
Napenda mtambue hii ni historia katika ukanda huu kuweza kutumia teknojia kufikia wanachama, Sisi ni wakisa sana tunaona mbele!.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya masoko na biashara Imani Kajula alisema.
‘Uanzishwaji wa Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa kuwamemba wa Simba, bali pia kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio yanayo andaliwa na Simba Sports Club. Pia maduka mbalimbali yatatoa punguzo kwa watoto wenye Simba Cub Card.
Wote mna jua fika kuwa mapenzi hujengwa, Simb aina lenga kujenga msingi imara wa kuendeleza wanachama na wapenzi wake’’.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za ki-elektroniki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa
kibiashara na klabu hiyo na Makamu wa Rais, Geofrey Nyange Kaburu.
Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa
kibiashara na klabu ya Simba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi hizo.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) akiwa na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa
kibiashara na klabu hiyo (kushoto) na Makamu wa Rais, Geofrey Nyange Kaburu wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za ki-elektroniki.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akimkabidhi kadi ya
uanachama wa Simba mtoto Terrence Peter wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za
kielektroniki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa
kibiashara na klabu hiyo.
Mussa Kova akipokea kadi yake mpya ya Ki-elektroniki kutoka kwa Rais wa Simba, Evans Aveva.
Viongozi wa Simba Evams Aveva (katikati) na Geofrey Nyange Kaburu pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula wakionyesha mfano wa kadi mpya za watoto chini ya miaka 18.
Watoto waliokabidhiwa kadi zao leo wakionyesha kadi walizokabidhiwa na uongozi wa Simba.
Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Simba baada ya kukabidhiwa kazi zao za kielektroniki.
No comments:
Post a Comment