Na Bryceson Mathias, Kilimani Dodoma
GHARAMA za Laki. 110,000/- kwa Fomu ya Udiwani, na Sh.600,000/- kwa Ubunge, zimewaudhi Watia Nia wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wasiokuwa na Kipato, kwamba kwa hatua hiyo, CCM kitakuwa Chama cha Ubaguzi, ambapo wasio na Kitu hawatakuwa Viongozi, isipokuwa Matajiri.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa Majina, Watia Nia hao waliojitokeza kuchukua Fomu jana kwenye Ofisi za CCM Dodoma Mjini, wamelalamikia, kuongezwa kwa gharama hizo wakidai, CCM Taifa kimeagiza, Sh. 10,000;- kwa Udiwani, na 100,000 kwa Ubunge.
“Hatuelewi kwa nini gharama zimebadilika Dodoma, wakati tuliowasiliana nao katika Mikoa mingine, hawana Gharama za namna hiyo, jambo ambalo tunaona kuna Agenda ya Rushwa, myuma yake, yenye lengo la kuwabeba wenye Uwezo, ili kututosa yusionacho tusichukue Fomu.
“Mjumbe wa Sekretarieti, Benjamini Kolimba, tulipomuuliza juzi kuhusu gharama hizo kwa wasio na Kipato alisema, twende kesho yake (asubuhi) na fedha za Fomu, lakini jioni tukashangazwa kuambiwa, Gharama za Ubunge ni Sh.2,000,000/-“.alilalamika mmojawao.
Mwandishi alimtafuta, Kolimba na kumhoji yeye ni nani, ambapo alisema yeye ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Mchakato huo, na alipobanwa ndani ya CCM ana Cheo gani alisema, ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi, si Katibu wa CCM wilayani humo anayetoa Fomu, ila aliyepo ni Mgeni, hayupo!.
Alipoulizwa sababu za gharama ya Laki 110,000/- kwa Udiwani badala ya 10,000/- na Laki 600,000/- kwa Ubunge alisema, ni gharama za kukodi Gari moja la kuwapeleka Watia Nia wote kwenye Jimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji kwa pamoja, ili kuondoa wasio na uwezo kuonekana hawana Usafiri.
“Mtu asiye na Fedha ya kuchangia Usafiri, hawezi kuzuiwa kuchukua Fomu au kuonekana hajatimiza Masharti, na kama atabebwa na Bodaboda, lazima aongozane na Gari hilo litakalokodishwa na kufika pamoja”.alisema Kolimba alipoulizwa kama mtu ana usafiri duni itakuwaje.
Aidha Wana CCM waliohojiwa, wamepinga gharama hizo wakidai, hata kama ukiamua Kuchapa Fomu ya kutia Nia ya Udiwani na Ubunge, haifiki hata Sh. 5,000/- hivyo, wamesema kuna Mchezo Mchafu unafanywa na Watendaji wa Mchakato huo, na kukitaka CCM kijitathimini.
No comments:
Post a Comment