Na Bryceson Mathias, Kibindu
KUTOKANA na Msakao Mkali wa
Magaidi uliokuwa ukiendelea kwenye Vitongoji na Vijiji vya Kibindu, Pera,
Kwaluhombo, Negelo na Vitongoji vinavyozunguka eneo hilo la Mapigono, Magaidi
waliojificha porini, wamelazimika kutimka na kutelekeza Vitabu, Sare, na Risasi
50 za Shortgun shambani.
Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, amesema, kutokana na Msako
Mkali unaoendelea katika Vitongoji na Vijiji ambavyo vilivamiwa na Maharamia
hao, Juzi baada ya kuzidiwa Mbinu walilazimika kukimbia na kuteleza Vitu hivyo
shamabani.
Alivitaja vitu hivyo kuwa
ni, “Sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (2), Bomu
lililotengenezwa (1), Risasi (50) za Bunduki (Shotgun),Fulana (3),Vitabu vya
Koran (2), Kisu-Jambia (1) na Begi (1), ambavyo vilifikishwa Polisi. alisema
Mgaza.
Polisi mkoani Pwani
imethibitisha kuokotwa kwa Vitu hivyo shambani, hivyo wamewaomba wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa makini kuokota vitu kama Bomu
wasivyovielewa isipokuwa watoe taarifa maeneo waliyotaarifiwa.
Habari toka kwa Mtendaji wa
Kijiji cha Pera,Mwanahawa Makani amesema, kuna watu wawili leo wamekuwa
wakioneka kwenye Kisima cha Maji shambani kwa mwananchi mmoja, hivyo kuwafanya
watu hasa akina Mama kuwa waoga kwenda kuchota Maji, lakini Polisi wa eneo la
tukio wamesema, Jambo hilo linafanyiwa kazi.
Hata hivyo kulikuwa na taarifa
zilizozagaa kwamba, katika Kijiji cha Pera kuna Wananchi watatu wameuawa na
Magaidi, lakini habari hizo zimekanushwa na Mtendaji Mwanahawa, akisema, Kuna
Magaidi Wawili ambao walikuwa wakingoja Wananawake kwenye Kisima.
Mwanahawa alipoulizwa iwapo
wananchi wanajitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kuduma la Wapiga Kura,
Mwanahawa alisema, “Watu wamejitokeza kwa Wingi na Wanaendelea kujitokeza bila
Woga wa Changamoto ya Magaidi hao, isipokuwa Mashine ndizo zinawaangusha hazina
Mtandao.
Wananchi waliohojiwa kwa
Nyakati tofauti akiwemo, Mama Judith Kamwana wamesema, “Hatuogopi kujiandikisha
kwa sababu ya Magaidi kwa sababu ua Ulinzi ambao Tangu awali tumeshuhudia,
Polisi ikishirikiana Vizuri na Viongozi na Wananchi, kutoa taarifa kila jambo
la ajabu linapotokea”.alisema Kamwana akiungwa Mkono na Wenzake.
No comments:
Post a Comment