HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2015

Mume Aua Mke naye ajinyonga

Na Bryceson Mathia, safarini Mbeya Vijijini.

MWANAUME, Tatu Anderson (33), wa Kitongoji cha Ilomba, Kijiji cha Jojo, Kata ya Santilya, Wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya, amemuua Mkewe, Veronica Tatu, kwa Kumvunja Shingo, na kisha naye akajinyonga kwa Kamba na Kanga.

Mtendaji Anderson Yamaleya, alisema Mwuaji alitenda Kosa hilo jana Oktoba 6, mwaka huu, kwa sababu ya Wivu wa Kimapenzi, ambapo baada ya kumpa Kipigo kikali, alimvunja Shingo, na kumfungia ndani akidhani amezirai.

Alisema, “Mwuaji alikuwa Mtengenezaji wa Mkaa, na inasemekana kuna mtu ambaye hajafahamika bado, alimpa taarifa kwamba, Mkewe wake ana uhusiano wa Kimapenzi na Mwanaume mwingine, jambo lililomuuthi, na aliporudi nyumbani alianza kumpiga mkewe kipigo kikali”.alisema Mtendaji

Mtendaji Yamaleya aliongeza, inadaiwa Mwanamke alipoona hali ni mabaya, aliamua kuondoka ili arudi kwao, na hapo ndipo Mwuaji alipongeza kipigo, kilichopelekea kumvunja Shingo, na alipoona hasemi alidhani amezirai, akaamua kumfungia ndani ili azinduke, na yeye akatoka!.

Mtendajia alisema, Mwuajia aliamua kuchukua Pikipiki ya ndugu yake ambayo namba zake hazikupatika na kuondoka;  Anasema wakati anaendesha, alianguka na kuumia vibaya, jambo ambalo wenzake walipomshauri akatibiwe, alisema atapona na kuamua kurudi nyumbani.

Alipofika nyumbani, alimkuta Mkewe amefariki muda mrefu, hivyo kwa hofu akaamua kukimbia nyumbani, huku akiwa amechukua Kamba na Kanga kuelekea kitongoji cha Itundu, ambako aliingia kwenye Nyumba isiyoisha (Pagare), na kujinyonga hadi kufa.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa Vifo hivyo viwili vya Tatu na Veronica, na kwamba Vijana wake (Polisi wa Upelelezi), wanaendelea na Kazi ya Uchunguzi, ili kumbaini aliyesababisha uchochezi wa Vifo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages