HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2015

Askofu; Kikwete Chukua Hatua, Usiwalalamikie Viongozi wa Dini

Na Mwandishi Wetu, Makambako, Njombe

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametakiwa kuchukua hatua dhidi ya Wagombea Urais wa Chama chake, wanaomwaga Mamilioni ya fedha kwa Vijana mikoani, badala ya kuwalalamika Viongozi wa Dini; Wakati Vyombo vyake vya Maadili kama TAKUKURU; Vikiwa Kimya!.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu, William Mwamalanga, wakati akifunga Kongamano la siku tatu la Maombi ya kuliombea Taifa linaloshirikisha Vijana wa Madhehebu ya Kikristo na Kiislamu wapatao3,000, lililofanyika Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe.

Askofu Mwamalanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Madhehebu ya dini, amemhimiza Kikwete, kuhakikisha ananuna wakati wa kujadili Majina ya wanaotaka Urais, huku wanaotumia Rushwa, ili majina yao yaondolewe,  arudishe Heshima ya CCM inayoporomoka kila kukicha.

Amesema, kutumia Fedha au Rushwa kuwahadaa Vijana ni Chukizo kwa Mwenyezi Mungu, kwani  Rushwa ni dhambi mbele za Mungu na ni machukizo  kwa wanadamu,  hivyo kumuunga mkono mtu wa jinsi hiyo  itakuwa ni kuhalalisha dhambi hiyo, jambo ambalo ni hatari kwa nchi.

Askofu Mwamalanga amemuasa Kikwete kwamba;  Hii ni mara ya kwanza kwa Wanasiasa kutafuta Urais Kibabe kwenye nchi ya Amani na yenye Mamilioni ya watu na wagombea  wengi,  jambo alilosema lianaashiria,Vurugu na Uvunjifu wa Amani.

Mwamalanga aliuza, “Mtu wa namna hii akishindwa kwenye Sanduku la kura, hawezi kutumia  Nguvu? Je hii siyo dalili ya Goli la mkono ambalo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kuwa CCM ipo tayari kufunga kwa goli la mkono? Alihoji Askofu mwamalanga

Askofu alibainisha kwamba, kutokana  na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao, wao kama Viongozi wa Dini; Hata kama mtu huyo anang'a kama Jua mchana, na kama Mwezi   Usiku, mtu wa namna hiyo siyo Kiongozi mzuri, bali analo kusudi baya kwa Taifa , hivyo hawezi kumuunga Mkono.

Alionya kuwa, kupitishwa kwa Mtumia rushwa yeyote kusaka Urais, kutaongeza Makundi ya Uhalifu, Mitatandao ya Ukabila, Utumwa, Mauaji ya wenye nacho na wasio nacho, na kujenga Magenge yanayokula kwa kuwalinda Matajiri,  hivyo mauaji ya albino na biashara ya mihadarati haviwezi kwisha nchini, ila zitaongezeka..

Nao Vijana wa Madhehebu hayo, Wamejigamba kuwa wametambua Mtego huo wa Panya, ambapo kwa Kauli moja wameaapa kutomuunga mkono Mgombea urais wa namna hiyo ambaye atakuwa Chukizo kwa Mwenyenzi Mungu kwani.

Aidha Vijana  hao 3,000 toka Shinyangaya Tanzania Bara, wamepongeza jitihanda za Kamati ya Maadili Amani  na Haki za binadamu kwa Madhehebu ya dini Nchini , kuwaweka pamoja kwa lengo la kuombea Taifa na kukuza akili  za kusimamia Amani na Uchaguzi unaokuja, hivyo wameazimia kuzunguka nchi nzima, ili kutangaza Wimbo wa kila Mtanzania wa kuwakataa watoa Rushwa.

No comments:

Post a Comment

Pages