HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2015

Mwanamke Aua Watoto Wawili na Jembe

Na Bryceson Mathias, Njeura na Mvomero

MWANAMKE wa Jamii ya Kimbulu wa Kijiji cha Njeura, Ester Daniel Maele (28) pichani, amewaua Watoto Wawili(2), baada ya kuwapiga kichwani na Jembe, wakati Mke mwenzie alipokwenda kujiandisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura ‘Biometric Voters Registration (BVR)’.

 Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Elizabeth Tesha, alithibitisha kupokelewa Maiti mbili za Watoto, Isaya Patrick(8) ambaye Mwili wake ulikutwa umening’inizwa ndani ya Nyumba, Paskalina Samwel(3), uliokutwa umelazwa Kifudifudi.   

Ester ambaye ametajwa na Wapenda Haki kuwa ni Mama mwenye Roho Mbaya, kwa sasa anashikiliwa na Polisi Mtibwa; Ingawa jana alikutwa amelazwa Hospitali ya Mtibwa akilindwa na asitoroke, kwa madai anaumwa Malaria Kali, jambo linalopingwa na Mashuhuda wa tukio hilo,

|”Tunalitaka Jeshi la Polisi, lisithubutu kutengeneza Mazingira ya Mchezo Mchafu wa kumponya Mama huyo Mwuaji, kwa kisingizio cha Ugonjwa wa Malaria Kali, kwa sababu inadaiwa Mama huyo aliwaua Watoto hao kwa Wivu wa kimapenzi, baina yake na Mke mwenzie.

“Tusingependa kuona Mbinu au Hila, ambazo awali Polisi ililalamikiwa kuwa, ilisababisha Vurugu na Migogoro ya Wakulima na Wafugaji, pale ilipodaiwa iliwakumbatia Wafugaji, Wakulima au Viongozi wa Serikali, kulikopelekea Mauaji, ambazo ni Nguvu Kazi ya Taifa, kama watoto hao ambavyo wangekuwa Viongozi”.alisema Mama aliyekataa kutaja jina.

Mbali ya Polisi kuthibitisha kumshikilia Mwuaji huyo, naye Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God wa eneo la tukio, (John Mathew) Jina linahifadhiwa, aliliambia gazeti hili kuwa, Awali ilidhaniwa, huenda Mauaji hayo yalikuwa yamefanywa na Magaidi, lakini ikabainika mwuaji alikuwa Ester!.

Hata hivyo alisema, Ester alipofanya Mauaji, alikimbilia porini, na alipoona Njaa, alikwenda kwa Mama wa Kimang’ati kuomba Chakula, huku akimtaka amuague asitambulike mwuaji, akimdhania ni Mganga wa Kienyeji, kumbe alikuwa mtu aliyefanikisha kukamatwa kwake.

No comments:

Post a Comment

Pages