Mwandishi wa Habari, Gordon Kalulunga akizungumza na
wananchi katika viwanja vya mahubiri Mjini Mbalizi wakati akitangaza nia ya
kugombea Ubunge jimbo la Mbeya vijijini (Picha na Kenneth Ngelesi)
NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MWANDISHI wa habari wa gazeti la
Mtanzania kutokaMbeya, Gordon Kalulunga amejitosa kuingia kwenye kinyang’anyiro
cha Ubunge katika Jimbo la Mbeya vijijini kupitia tiketi ya Chama cha
Mapinduzi(CCM).
Kalulunga ambaye pia ni mlimikio
wa Blog ya Kululunga Blog alitangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea
kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao
kwwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana kwenye viwanja vya
mahubiri Mbalizi mkoani Mbeya.
Mtia nia huyo alisema endapo Chama
chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha
wananchi wote wanajiunga na mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya matibabu kwa
kila kaya kuchangia ili kupunguza adha na gharama kubwa za matibabu.
Aliongeza endeapo atafanikiwa
kuukwaa Ubunge atahakikisha anasimamia
na kupigania jimbo hilo liweze kupata chuo cha fani yoyote ili kuwawezesha
ajili ya vijana kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira
kwa vijana.
Kalulunga alisema kipaumbele
kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kupigania ujenzi wa ofisi za makao
makuu ya Wilaya hiyo katika eneo husika ili kurahisisha upatikanaji wa huduma
kwa wananchi tofauti na ilivyosasa ambapo Ofisi za Wilaya ya Mbeya zipo
katikati ya Jiji la Mbeya.
Awali Katibu wa Umoja wa vijana
chama hiccho Wilaya ya Mbeya vijijini (UVCCM),Japheti Siulanga aliwataka vijana
wamuunge wamuunge mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka
kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.
Aidha katika mkutano huo vijana
zaidi ya 26 walijiunga na Chama cha mapinduzi na kukabidhiwa kadi za umoja
wa Vijana.
No comments:
Post a Comment