HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 11, 2015

TANO BORA WA CCM HAWA HAPA

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma akidhibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa katika mitandaoni ya kijamii juu ya wagombea waliopita katika tano bora ambapo aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali, Majina hayo yanapekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndiye atakuwa mgombea Urais.   (Kwa hisani ya Michuzi Media)
Waandishi wa habari wakiwa nje ya ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Pages