HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 18, 2015

PSPF KUKOPESHA VIWANJA WANACHAMA WAKE KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA POSTA, PROPERTY INERNATIONAL LTD

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akizindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania na Taasisi ya Property Intarnational Ltd. Wengini kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Fedha wa PIL, Hashimu Thabit, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Gabriel Silayo,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Haleem Zahraan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Gabriel Silayo akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Haleem Zahraan akitoa hotuba yake.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa uzinduzi.
 Wafanyakazi wa Property International wakiwa katika uzinduzi.
 Wafanyakazi wa PIL na wageni waalikwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Benki ya Posta Tanzania na Property International Ltd. 
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia).
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia).
 Wafanyakazi wa Property International Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia).
 Wasanii wa kikundi cha Mjombamjomba wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia waliokaa).

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, amewahimiza wanachama wa mfuko wa PSPF na watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa ya mikopo
ya viwanja inayotolewa na mfuko huo.

PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB) na kampuni ya Property International, wameingia makubaliano ya kukopesha wanachama wake viwanja, ili waweze kuwa na makazi bora.

Akizundua mpango huo jijini Dar es Salaam, Samia ambaye pia mgombea mwenza wa Urais wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema mpango huo utaondoa usumbufu kwa wananchi kwa kuwa watapatiwa viwanja vilivyopimwa.

“Kwa kuwa asilimia kubwa ya wanachama wa PSPF ni walimu, hivyo mpango huu pia itasaidia kuondoa kero za nyumba kwa walimu na pia serikali itaweza kukusanya kodi, kwa sasa inakosa fedha nyingi kutokana na kuwepo kwa makazi holela,” alisema.

Awali, Mkuruenzi wa Mpango na Uwezezaji wa PSPF, Gabriel Silayo, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, alisema mwanachama atakayefaidika na mpango huo ni yule aliyechangia kwa zaidi ya miezi sita na kwamba mkopo huo ataulipa ndani ya miaka mitatu.

“Tuna wanachama zaidi ya 350,000 na wengi wao ni walimu, hivyo naamini tutatatua kero ya nyumba kwa walimu,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TPB Sabasaba Moshingi, alisema hiyo ni fursa nzuri, ili nchi iweze kuwa na miji iliyopangwa, hivyo tupo tayari kutoa mikopo kwa wanachama wa PSPF,” alisema.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Property International, Abdulrahim Zahran,  alisema watawahudumia wananchi kwa kuwapatia viwanja vilivyopomwa ambavyo pia vitakuwa na hatimiliki.

No comments:

Post a Comment

Pages