HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 29, 2015

274 WASHILIKILIWA KWA VURUGU MBOZI NA RUNGWE

Na Kenneth Ngelesi, MBEYA

WATU 274 wanashikiriwa na jeshi la Polisi Mkoani  wakitumiwa kufanya vugugu na kusababisha uvunjifu wa amani siku ya uchaguzi Mkuu katika Majimbo ya Uchaguzi ya Vwawa,Mbozi na Rungwe.

Taarifa ya kukamatwa zilitolewea jana na kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ahamed Msangi wakati akitoa taaarifa kwa waandishi wa habari juu ya vurugu zilizotokea katika majimbo yote matatu.

Akizungumza na Waandishi Kamanda Msangi alisema kuwa Oktoba 25 majira saa 10:00 katika majimbo hayo kwenye miji ya Vwawa na Mlowo katika Wilaya ya Mbozi na na pika katika miji ya Tukuyu na Kiwira Wilaya ya Rungwe walijitokezaa vijana wakishinikiza kutangaziwa matokeo ya Ubunge.

Alisema kuwa wakati zoezi la kuhesaba na kujumlisha kura likiendelea katika Mji wa Vwawa lilitokea gari lililokuwa na vifaa vya kupigia kura lilinaingia katika ofisi ya Mkurugenzi Mbozi ambaye ndiye msimamizi wa Uchaguzi maali ambapo  zoezi la kuhesabu kura lilikuwa likiendelea.

Msangi alisema kuwa baada wananchi kuliona gali hilo walijawa na hasira na kuanza kurushia mawe kwali walikuwa wakilitilia shaka kuwa huenda lilikuwa na kura feki.

Alisema baada ya kurusha mawe kwenye gali hilo ambalo hata hivyo hakuweza kutaja namba za usajili wa gari lilihaibika na kuvunjwa vioo.

Mbali na kurusha mawe katika gari hilo alisema kuwa ilipofika majira ya saa 1:00 jioni wananchi waliziba njia zote katika miji hiyo ya Vwawa na Mlowo kwa kapanga mawe na kuchomo moto matairi kwa lengo la kutaka matokeo yatangazwe.

Alisema baada ya kuona vurugu hizo zinazidi nashughuli mbalimbli zimesimama ukiwepo usafri wa barabara kuu ya Tanzania -Zambia Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWT waliaanza kuwa tawanya wananchi hao ambao anadaiwa kuwa ni wafausi wa chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema)

Aidha kamanda Msangi alisema kuwa licha ya kutokea kwa vurugu hizo lakini pia kulitokea na uahabifu mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchomwa moto kwa Ofisi ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mbozi, na ofisi ndogo ya chama hicho  tawi la Mlowo pamoja na mahakama ya mwanzo Mlowo.

Aidha Msangi alisema kuwa mbali ya hilo lakini pia vuruvgu hizi zilisababisha uhabifu mkubwa wa mali uakiweomo magari matano ambapo mengine yalichomwa moto na mengine kuvunjwa vioo vya magari amabyo yalikuwa yameegeshwa katika Hotel ya Califona Mjini Mlowo ambayo inatajwa kuwa ni mali ya rafiki wa zambiana kwamba wafuasi wengi wa caham cha mapinduzi wamekuwa wakifanyia vikao.

Mbali na uharibu wa vitu hivyo lakini pia uhabbifu wa miundo mbinu ya barabara za Miji hiyo pamo ja barabara kuu ya kulekea katika nchi jirani ya Zambia kwa upande wa Mbozi na barabara ya Tanzania na Malawi kwa upande wa Rungwe.

Alisema kuwa kutokana hali Jeshi la Polisi kwa kushirikina na Jeshi la wananchi wamefanikiwa kuwa kamatu watu hao na kwamba bado wanaendElea na msako wa kuwa tafuta watu wengine walio shiriki katika vurugu hizo.

Msangi alisema kuwa baadhi yao wamesha fikishwa Mahakama ya Wilya ya Mbozi na Wengine Mbeya mjini, kwa ajili ya kujibu tuhumu zinazo wakabili zikiwemo za kufanya vuguru na kusababisha uvujifu wa amani kinyume cha sheria na uharibifu wa mali.

Aidha Kamanda masangi alisema kuwa kati yao 158 walikamatwa jimbo la Rungwe ambapo ambao walikuwa wakishinkiza matokeo ya Ubunge ambapo katika jimbo hilo kulikuwa namvutano mkali kati ya wafusa ya Chadema walikuwa wakiamini mgombea wao John Mwambija kashinda na wakati huo chama cha mapinduzi  CCM nao wakiwa na imani kuwa mgombea wao  Saul  Amon ndiye mshindi harali.

Wakati huo huo watu 116 walikamatwa katika majimbo wawili ya Mbozi na Vwawa katika Wilaya ya Mbozi ambao nao walikuwa wakitaka kutangaziwa matokeo ya uchaguzi Jimbo la Mbozi ambapo Mchuani mkali ulikuwa kati ya Pasco Haonga wa Chadema ambaye ametangazwa mshindi alikuwa akichuna na naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi ambaye amaeungaka.

Katika jimbo la Vwawa mchuano mkali ulikuwa kati ya Jesefat Hasunga wa chama cha Mapinduzi na Fanuel Mkisi wa (chadema) ambpo Mkuregenzi wa uchaguzi Edina Mwaigomole alimtangaza Hasunga wa CCM kuwa mshindi.

Msangi alisema kuwa mbali na watu hao kushikiriwa lakini pia jumla ya pikipiki 30 zinashikiliwa na Jeshi hilo ambazo zilitekelekezwa na watu wasiojulikna baada ya kutokelea vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages