Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akikata keki na mmoja wa
wateja wa Benki hiyo tawi la Oysterbay wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki
ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimlisha keki mmoja wa wateja
waliofika kupata huduma katika tawi la CRDB Oysterbay jijini Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Oysterbay, Juliana Mhimbira.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimlisha keki mmoja wa wateja
waliofika kupata huduma katika tawi la CRDB Oysterbay kama ishara ya
kuwashukuru wateja wa Benki hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya
Huduma kwa Wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akisikiliza maoni ya
mteja mkubwa wa Benki ya CRDB tawi la Oysterbay jijini Dar es Salaam, mwishoni
mwa wiki, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na wateja wa Benki ya
CRDB tawi la Oysterbay jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa
kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba Upendo Assey wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Dk. Charls Kimei akisalimiana na wateja.
Dk. Charles Kimei akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB.
Dk. Kimei akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba Upendo Assey wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Dk. Charls Kimei akisalimiana na wateja.
Dk. Charles Kimei akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB.
Dk. Kimei akizungumza na waandishi wa habari.
‘Tumerejesha bil. 1.3/- kwa jamii’
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema
benki yake imetumia sh bilioni 1.3 ikiwa ni sehemu ya faida yake, kurejesha kwa
jamii kupitia sekta ya elimu, afya na mazingira.
Alizungumza hayo akiwa na baadhi ya wateja wa benki hiyo Tawi
la Oysterbay mwishoni mwa wiki wakati wa hitimisho la Wiki ya Huduma kwa Wateja
wa CRDB nchini kote.
“Oktoba ya kila mwaka tunatumia wiki hii kurejesha asante
yetu kwa jamii, tumegawa madawati katika shule mbalimbali za msingi yenye
thamani ya zaidi ya sh. milioni 40 kwa shule mbalimbali za msingi hapa nchini.
“Manispaa ya Kinondoni tumepeleka dawa na vitendanishi kwa
ajili ya kipindupindu vyenye thamani ya sh. milioni 15 pamoja na shughuli
nyingine nyingi zilizofanywa na watumishi wetu kwenye matawi yetu yote,” alisema
Dk. Kimei.
Alisema umuhimu wa wiki ya huduma kwa wateja ni kuboresha
ufanisi wa utendaji na huduma kwa kuwa ni kipindi cha wateja kueleza kero,
maoni na ushauri wao kwa uwazi.
Wiki ya huduma kwa wateja wa CRDB huadhimishwa kuanzia
Oktoba 5 hadi Oktoba 11 ya kila mwaka ambapo wafanyakazi wa benki hiyo hufanya
shughuli mbalimbali za kijamii.











No comments:
Post a Comment