Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Urais Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Samia Hassan Suluhu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu katika hafla hiyo.
Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment