Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa vyama
vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto) na baadhi ya wajumbe
wa Ofisi hiyo. Kushoto ni msajili wa vyama Zanzibar Bw. Rajab Baraka.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akigana na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania
Jaji Francis Mutungi baada ya mazungumzo yao, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akigana na baadhi ya wajumbe wa Ofisi ya Msajili
wa vyama vya siasa Tanzania baada ya mazungumzo yao, nyumbani kwake Mbweni
Zanzibar.
Na Talib Ussi, Zanziabar
Msajili wa vyama vya
siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa vyama
vya siasa Zanzibar kukutana, ili kutatua mzozo wa kisiasa uliojitokeza.
Amesema Zanzibar ni
nchi amani, hivyo hakuna haja ya kuruhusu migogoro ya aina hiyo ambayo inaweza
kupelekea kuvurugika kwa amani na kuipotezea sifa Zanzibar katika jamii ya
Kimataifa.
Jaji Mutungi
akiambatana na baadhi ya wajumbe wa ofisi hiyo ya msajili pamoja na msajili wa
vyama kwa upande wa Zanzibar Bw. Rajab Baraka, ametoa ushauri huo wakati
akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema kuna kila
sababu ya kulinusuru taifa kuingia katika migogoro isiyokuwa ya lazima, na
kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kumaliza tatizo hilo.
Kwa upande wake
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia
ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, amesema amekuwa akichukua juhudi
binafsi kukutana na wagombea wenzake kuzungumzia tatizo hilo, lakini baadhi yao
wanaonekana kutokuwa tayari kulizungumza.
Amesema hapendi kuona
Zanzibar inaingia katika machafuko yanayoweza kuepukwa, na kwamba viongozi
wengine pia wanapaswa kufikiria amani na maslahi ya Zanzibar kuliko maslahi
binafsi.
Katika hatua nyengine
Maalim Seif amemshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bw.
Jecha Salim Jecha kwa kuiingiza nchi katika migogoro ya kisiasa na kikatiba.
Akinukuu vipengele
vya Katiba ya Zanzibar, Maalim Seif amesema kipindi cha Urais wa Zanzibar ni
miaka mitano kuanzia tarehe ya kuapishwa, hivyo kuanzia tarehe 02/11/2015
kipindi cha Urais wa Zanzibar awamu ya saba kitakuwa kimemalizika.
No comments:
Post a Comment