HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 15, 2015

MAPOKEZI DIAMOND BALAAA

 Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Nassib Abdul 'Dimond Platinumz' akiwa ameshika mojo kati ya tuzo tatu alizotwaa za Afrimma mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo akitokea Marekani. (Picha na Francis Dande)
Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Nassib Abdul 'Dimond Platinumz' akisindikizwa na mashabiki kwa miguu mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’, leo amepata mapokeza ya aina yake kutoka kwa mashabiki wake wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Diamond aliwasili majira ya mchana akitokea nchini Marekani ambako alitwaa tuzo tatu za Afrimma.

"Nawashukuru wale wote walionisapoti mpaka kufikia hatua hii" alisema Diamond wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa atahakikisha anajituma zaidi ili kutoa nyimbo kali zaidi.

Msafara wa Diamond ulitoka Uwanja wa Ndege kwa miguu kuelekea nyumba kwao Tandale na baadae katika Ufukwe wa Esca One ambapo alitarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wake na watanzania kwa ujumla baada ya kutwaa tuzo hizo.

Hata hivyo msafara wake ulishindwa kuendelea na safari kwa miguu baada ya Polisi kuuzuia katika eneo la Vingunguti na kumolazimisha msaii huyo kupanda gari.

No comments:

Post a Comment

Pages