Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria (The Desert Warriors) pichani unatarajiwa
kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na
jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi
Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
Kocha mkuu wa timu hiyo Iitakayofikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt
Kempsinki, Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha
wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa
ajili ya kuikabili Tanzania.
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda mlango, Doukha
Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR
Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor),
Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy
(Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples),
Mandi Aissa (Reims).
Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller),
Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil
(Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad
(Leicester).
Washambuliaji Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon),
Belfodil Ishak (Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah
Baghdad (Etoile du Saleh)
No comments:
Post a Comment