HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2015

DK. KIMEI AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA SIHA SANGO


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika ibada maalum ya harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Siha Sango Mkoani Kilimanjaro ambapo zaidi ya shs. milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo. (Picha na Francis Dande)
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango, Cuthbert Temba akitoa mahubili wakati wa ibada maalum ya harambee ya uchangiaji wa kanisa hilo.
 Waamini wakiwa katika ibada.

NA MWANDISHI WETU, SIHA

MKURUGENZI wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amewaongoza waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Siha Sango kuchangisha fedha na kupata zaidi ya sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya.

Katika harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika kanisa hilo mkoani Kilimanjaro, Dk. Kimei aliwapongeza waamini hao kwa kupata moyoa wa kujenga nyumba ya Mungu.

“Mimi sio mwanasiasa pengine nitakua mwanaisasa baadae lakini sio sasa… nimefurahi kualikwa hapa na nimebahatika kukanyaga kanisa hili kabla halijabomolewa.

“… Ni kanisa la zamani limechakaa, mmeliona hili nawapongeza kwa kuamua kujenga jingine jipya,” alisema Dk. Kimei aliyeongozana na baadhi ya watumishi wa benki hiyo.

Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Siha Sango, Cuthbert Temba aliwataka waamini na watanzania kufanya shughuli za maendeleo kwa nchi baada ya uchaguzi mkuuu kumalizika kwa amani.

“Nawaomba watanzania wote tushirikiane, tufanye kazi za ujenzi wa taifa hili kwa lengo la kujiletea maendeleo ya kiuchumi, uchaguzi umeisha salama sasa tujenge taifa na nyumba ya Mungu,” alisema Mchungaji Temba.

Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango lilijengwa mwaka 1916 hivyo limechakaa, waamini wa kanisa hilo walikubaliana kujenga kanisa jipya kwenye eneo hilo litakalogharimu sh milioni 200.

No comments:

Post a Comment

Pages