Irene Mrema
aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia
promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania (kushoto)
akimwelezea Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kulia)alipomtembelea
nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake
likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya
Goba jijini Dar es Salaam.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akisalimiana na Irene Mrema
aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia
promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo, Alipomtembelea
nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake
likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya
Goba jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Mmoja ya washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia
promosheni ya Jaymillions iliyokuwa inaendeshwa na Vodacom Tanzania
iliyomalizika mwezi Aprili mwaka huu Irene Mrema, amesema tangu aibuke na
ushindi amepata mafanikio makubwa mojawapo ikiwa ni kuweza kujenga nyumba ya
kuishi na familia yake maeneo ya Goba nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam.
“Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunikwamua kimaisha kupitia
Jaymillion ya Vodacom kwa kuwa imeleta mafanikio makubwa katika maisha yangu na
familia yangu kwa kuwa imetuwezesha kujenga na kumiliki nyumba nzuri ya kisasa
ambayo tayari tumehamia pamoja na familia yangu”.Alisema
Mbali na ujenzi wa nyumba hiyo Irene Mrema alieleza kuwa hivi
anajipanga kufungua biashara ambayo bado anaifikiria kwa fedha
alizosalia ili kuwezesha kukuza kipato cha familia “Natarajia kufungua
biashara katika siku za hivi karibuni kwa ajili ya kuniwezesha kijitegemea na
kuongeza kipato cha familia”
Aliishukuru kampuni hiyo kwa kubuni promosheni zenye kuboresha maisha
ya wateja wake na kuongeza kuwa fedha hizo alizoshinda zimeweza kusaidia katika
mambo mbalimbali ya kijamii na akifungua biashara atatoa ajira kwa wafanyakazi
ambao nao watanufaika na ushindi wake.
”Mafanikio haya ambayo yanaonekana kwangu kama ndoto ukimwelezea
mtu anaweza akashindwa kuamini hususani wale ambao wanakuwa na dhana kuwa
promosheni za makampuni kwa wateja kama ilivyokuwa Jaymillion ni za uongo
lakini napenda kuwahakikishia kwamba
hakuna uongo,upendeleo wala kujuana bali ni bahati ya mtu na
akishinda anapewa fedha zake kama ilivyotokea kwangu”.Alisema Irene
kwa furaha.
Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambaye
alifanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya washindi wa promosheni hiyo alisema
amefurahishwa na hatua aliyofikia mshindi huyo ya kupiga hatua ya kimaendeleo
kimaisha.
“Kwetu Vodacom mafanikio haya ya mteja ni faraja kubwa kwa kuwa
mbali na kutoa huduma bora na kubuni huduma za kurahisisha maisha ya wateja pia
ni kufanya maisha ya wateja wetu kuwa murua kupitia promosheni zetu”.Alisema
Nkurlu.
Alisema promosheni za kukwamua maisha ya wateja zikiwa na tija na
kuleta mafanikio kwa wateja zinahamasisha kampuni kuendelea kubuni promosheni
zingine ili ziweze kubadilisha maisha ya wateja wengi zaidi
Alimalizia kwa kuwataka wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa mbalimbali
zinazotolewa na kampuni hiyo na zitakazokuwepo katika siku za usoni.
No comments:
Post a Comment